Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:26

Mawaziri watatu wateule wa Trump waendelea kuhojiwa na kamati za seneti


Jenerali mstaafu James Mattis akiwa mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi. Jan. 12, 2017.
Jenerali mstaafu James Mattis akiwa mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi. Jan. 12, 2017.

Carson aliwahi kupinga programu ya serikali ambayo alisema inaendekeza “utegemezi,” na ameendelea kunadi kuwa sifa ya kila mtu kufanya kazi kwa bidii iwe ni kigezo cha mafanikio

Chaguo la rais mteule, Donald Trump kwa mtu ambaye ataongoza Wizara ya Ulinzi ili kupitishwa, kuongoza wizara hiyo, mstaafu Jenerali James Mattis anatoa ushuhuda wake leo Alhamisi mbele ya kamati ya seneti ya huduma za kijeshi ambayo inategemewa kumpitisha.

Mattis atakuwa ni mwanajeshi wa kwanza katika jumuiya ya jeshi atakayeongoza Pentagon baada ya zaidi ya miaka 50. Alistaafu kutoka katika kitengo cha Marine mwaka 2013 baada ya kufanya kazi kama kiongozi wa kituo cha Central Command, ana uzoefu wa kuongoza majeshi wakati wa vita vya Afghanistan na vita vingine viwili nchini Iraq.

Ni nadra hili kutokea

Lakini sheria inawazuia maafisa wa jeshi kuwa mawaziri wa ulinzi mpaka kipite kipindi cha miaka saba baada ya kustaafu kwao, hivyo bunge la Marekani litalazimika kupitisha uteuzi huu ikiwa ni hali ya kipekee kwa mara hii.

Sheria hiyo iliyoandikwa mwaka 1947, ilikusudia kuwawezesha watu wanaotoa huduma za kijeshi na wale wanaongoza idara za serikali kuweza kutumikia nafasi hiyo.

Kamati ya huduma za jeshi imepangwa kulizungumzia suala hili ambalo ni nadra kutokea mara tu baada ya jina la mteule huyu kupitishwa.

Mattis amekuwa akieleza mashaka yake juu ya Iran ilivyokuwa tishio kwa dunia na hakubaliani na mbinu za hali ya juu za kupata taarifa kwa kumtesa mshukiwa kwa kutumia maji maarufu kama 'waterboarding.'.

Uteuzi wa mkuu wa CIA
Mteule wa Trump kwenye nafasi ya CIA, ambaye ni mwakilishi wa Republikan katika bunge, Mike Pompeo atahojiwa Alhamisi mbele ya Kamati maalumu ya upelelezi ya seneti ili kuthibitishwa.

Pompeo amekosoa uongozi wa rais Barack Obama kwa kushambulia mbinu za kuhoji wahalifu, akisema taratibu hizo zilikuwa “ndani ya sheria, katika katiba na zilifanyika kwa ufahamu kamili” wa mawakili wahusika.

Pompeo ambaye ni msomi wa Havard katika shule ya sheria na chuo cha kijeshi cha West Point, alisababisha utata mwaka 2013 baada ya kupendekeza viongozi wa kiislamu ambao hawalaani waziwazi mashambulizi ya kigaidi “wana uwezekano wa kuwa washiriki” katika mashambulizi hayo.

Trump mara nyingi amekosoa idara za kipelelezi na ameshuku kuwa idara hizi zilihusika kuvujisha madai yasiyoweza kuthibitishwa juu ya mahusiano yake na Russia. Rais mteule amesema wakati akimteua Pompeo atakuwa ni "kiongozi hodari na shupavu kwa jumuiya yetu ya kipelelezi.”

Uteuzi wa Ben Carson

Kiongozi wa tatu kuthibitishwa baada ya kuhojiwa Alhamisi inamhusisha mmoja wa wapinzani wake Trump katika kinyang’anyiro cha kuwania urais, mstaafu mtaalamu wa upasauji, Ben Carson ambaye anatarajia kuongoza wizara ya makazi na maendeleo ya miji (HUD).

Baada ya Trump kushinda katika mchakato wa kutafuta mgombea wa Republikan, baada ya takriban mwezi mmoja Carson alitangaza na yeye kuingia katika mbio hizo za urais, na alikuwa ndiye mpinzani pekee aliyeweza katika anga za Republikan kumtangulia katika kura za maoni kitaifa, japokuwa hilo lilidumu kwa muda mfupi. Carson alimuunga mkono Trump baada ya kujitoa katika kinyang'anyiro hicho.

Dr. Ben Carson iakiapishwa kabla ya kutosha ushuhuda kwenye kamati inayosikiliza uteuzi wake. Jan. 12, 2017.
Dr. Ben Carson iakiapishwa kabla ya kutosha ushuhuda kwenye kamati inayosikiliza uteuzi wake. Jan. 12, 2017.

Hata hivyo Carson hana uzoefu wa huduma za umma, lakini mkusanyiko wa mawaziri waliofanya kazi katika wizara hiyo ya HUD chini ya uongozi wa Bill Clinton na George W. Bush waliandika barua kwa kamati inayomhoji kusema wanaamini atasikiliza idara ya wafanyakazi wa serikali na kuwawezesha katika hatua zao za kujenga nyumba za bei nafuu zenye kulingana na uwezo wa wananchi na zinazojumuisha jamii zote za wamarekani.

Siku za nyuma Carson aliwahi kupinga programu ya serikali ambayo alisema inaendekeza “utegemezi,” na ameendelea kunadi kuwa sifa ya kila mtu kufanya kazi kwa bidii iwe ni kigezo cha mafanikio.

XS
SM
MD
LG