Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:29

Jopo la Seneti: Russia itamulikwa popote uchunguzi utakapotufikisha


Seneta Richard Burr
Seneta Richard Burr

Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti la Marekani itaiangaza Russia Alhamisi wakati inakutana katika kikao chake cha wazi ikiwa ni sehemu ya kusikiliza madai kuwa Russia ilivuruga uchaguzi wa urais Novemba.

Kamati hiyo pia itaangalia kama kulikuwa na msaada wowote walioupata Russia kutoka katika duru za ndani za Rais Donald Trump.

Kamati hiyo imeelezea kikao hicho cha Alhamisi ni sehemu ya maandalizi ya historia na tabia ya “harakati na ushawishi wa vitendo wa kampeni za Russia,” na uwezo wa nchi hiyo katika masuala ya kimtandao.

Kabla ya mahojiano ambayo yanafuatiliwa kwa karibu na umma, mwenyekiti wa kamati hiyo Mrepublikan na kiongozi wa juu Mdemokrat wameahidi kufanya uchunguzi wa kina na usio na upendeleo juu ya juhudi za Russia katika kuvuruga kampeni ya mwaka jana.

“Upeo wa uchunguzi huu utakwenda upande wowote ambao uchunguzi utajielekeza,” Mwenyekiti Richard Burr, Mrepublikan anaewakilisha North Carolina, amesema katika mkutano na waandishi Jumatano.

“Tutatafikia undani wa uchunguzi huu,” alikubaliana Seneta Mark Warner wa Virginia, kiongozi wa juu Mdemokrat wa kamati hiyo.

Burr amesema kuwa “nyaraka nyingi zilizokuwa hazipo” zimepokelewa na kamati, na kamati iko katika “mfululizo wa mazungumzo” na jumuiya ya wapelelezi ili kuweza kupata nyaraka zaidi.

Amesema kuwa kutakuwa angalau na mahojiano yasiopungua 20, ikiwa pamoja na kumhoji mshauri na mkwe wake Rais Trump, Jared Kushner, ambaye amekubali kuzungumza na jopo la kamati hiyo.

“Kamati itafanya mahojiano na Kushner wakati itapokuwa tayari imeamua muda mwafaka kupanga tarehe ya mahojiano hayo,” amesema mwenyekiti.

Haikuwa Burr wala Warner aliyetoa hitimisho lililofikiwa mpaka sasa, isipokuwa kueleza makusudio ya Russia.

“Lengo la Vladimir Putin ni kuiona Marekani iliyotetereka,” Warner amesema. “Ikiwa dhaifu kiuchumi, na kimataifa. Na hilo lazima liwe linamshughulisha kila Mmarekani bila ya kujali mrengo wa chama chake.”

Mpaka sasa, Kamati ya Usalama ya Bunge ilikuwa inaongoza katika uchunguzi wa Russia.

Lakini kamati hiyo ilisitisha kusikiliza mahojiano ya wazi wiki hii baada ya kuzuka mzozo uliomhusisha mwenyekiti wake, Mbunge wa Republikan, Devin Nunes, ambae alimpa Rais Trump muhtasari wa nyaraka za siri ambazo alikuwa hajaziwasilisha katika kamati.

XS
SM
MD
LG