Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 16:23

Saudi Arabia yavunja uhusiano na Iran


Waandamanji wa kishia
Waandamanji wa kishia

Khamenei alisema kuwa, ni makosa pia kwani damu iliyomwagika bila shaka italeta ulipizaji kisasi wa halali.

Mzozo unaendelea kati ya Saudi Arabia na Iran, ambapo jana serikali ya Riyadh imevunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Tehran siku moja baada ya waandamanaji kutia moto ubalozi wa Saudi Arabia katika mji mkuu wa Iran.

Wachambuzi wanasema mvutano kati ya mataifa haya mawili makuu ya Mashariki ya Kati Saudi Arabia na Iran unatia wasi wasi na huwenda ukazorotesha ugomvi wa kidini kati ya Washia na Wasuuni duniani.

Akitangaza uwamuzi wa kukata uhusiano wa kidiplomasia jana jioni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Saudi Arabia Abdel al-Juberi, amesema ni lazima kwa wanadiplomasia wote wa Iran waondoke nchini humo katika muda wa saa 48 zijazo.

"Tunadhamira ya kutoruhusu Iran kuhujumu usalama wa nchi yetu. Tunadhamira ya kutoipatia Iran nafasi ya kujipanga au kubuni vikundi vyua kigaidi hapa nchini au katika nchi nyingine shirika.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Lou Lorscheider, anaripoti kwamba ugomvi huo ulianaza muda mfupi tu baada ya maafisa wa serikali ya Saudia mkutangaza jumamosi kwamba wamemnyonga imamu mashuhuri wa kishia mkosowaji mkuu wa utawala wa kifalme wa Saudi Arabia Shiek Nimr al-Nimr pamoja na washia wengine 47.

Al-Nimr alihukumiwa mwaka 2014 kwa tuhuma za uchochezi na mashtaka mengine ya kigaidi akiwa kiongozi mkuu wa maanamano ya washia mwaka 2011 huko amshariki ya Saudi Arabia.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Tangazo la mauwaji ya watu hao yalizusha mara moja hasira na lawama kutoka pembe mbal;I mbali za dunia hasa nchi za kislamu.

Kiongozi wa kidini wa Iran Ayatollah ali Khamenei ameeleza mauwaji hayo kuwa ni uhalifu mkubwa.

"Ni makosa pia kwani damu iliyomwagika bila shaka italeta ulipizaji wa halali. Alisema wanasiasa wa Saudia Arabia, watawala pamoja na wapanga sera wasiwe na shaka kwamba watalipizwa kisasi kwa umwagikaji huo wa damu."

Haijajulikana wazi ulipizaji kisasi huo utafanyika namna gani.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imetoa taarifa inayoeleza kwamba serikali ya Washington itaendelea kuwahimiza viongozi wote katika kanda hiyo kuchukua hatua thabiti kupunguza mvutano. Ikieleza kwamba serikali ya Obama inaendelea kuamini mashauriano ya kidiplomasia na mazungumzo ya ana kwa ana ni muhimu katika kutanzua mzozo huo.

Maandamano yamefanyika katika miji mbali mbali ya nchi za kislamu kulaani mauwaji hayo.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amesema amechukizwa sana na kuuliwa kwa Sheik Nimr na kutoa wito wa utulivu na kustahmiliana kutokana na mauwaji hayo.

XS
SM
MD
LG