Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:52

Umoja wa nchi za kiarabu waitaka Iran kupunguza mivutano na Saudia.


Waziri wa nchi za nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir akihuduria mkutano wa umoja wa kirabu mjini Cairo, Egypt.
Waziri wa nchi za nje wa Saudi Arabia, Adel al-Jubeir akihuduria mkutano wa umoja wa kirabu mjini Cairo, Egypt.

Rais wa Iran Hassan Rouhani wiki ilopita alilieleza shambulizi la ubalozi wa Saudi Arabia, kuwa ni kosa na ni kinyume cha sharia. Lakini anasema Saudi Arabia haiwezi kutumia kisingiuzio cha kuvunja uhusiano wa kibalozi na Iran, kuficha uhalifu wake.

Mawaziri wa nchi za nje wa umoja wan chi za kiarabu walielezea uungaji mkono wao na Saudi Arabia, wakati wa mkutano hiyo jana mjini Cairo kujadili mashambulizi kwenye ofisi za ubalozi wa Saudi huko Iran. Mataifa manane ya kiarabu yamepunguza uhusiano na Iran kufwatia kuuliwa kwa sheke wa kishia na Saudi Arabia.

Mawaziri na wanadiplomasia wa umoja wa nchi za kiarabu walokusanyika Cairo, walipiga makofi pale waziri wa masuala ya nchi za nje wa umoja wa falme za kiarabu Sheik Abduallah bin Zayid alipoishambulia Iran.

Sheik bin Zayid alidai kwamba , Iran inatumia suala la madhehebu kama chombo cha uwongozi wake dhidi ya kanda hiyo na kuingilia kati masuala ya ndani ya mataifa ya kiarabu. Anasema, Iran inaunga mkono makundi yenye itikadi kali. Inawapa mafunzo na kuwapatia magaidi silaha na kuunda makundi ya wanamgambo ili kueneza ghasia na kuleta ukosefu wa uthabiti katika kanda hio.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Adel Al Jubeir, aliishutumu Iran kwa kuwaandikisha majasusindanmi ya nchi za kiarabu na kuwatumia dhidi ya serikali zao na kuihimiza kusita kuingilia kati masula ya ndani ya jirani zake.

Adel Bin Al Jubeir anadai Saudi Arabia haitaki kuwepo kwa mzozo wa Kisunni na kishia, lakini anasema, Iran ilianza kupanda mbegu za mgawanyiko wadini baada ya mapinduzi yake ya mwaka 1979, wakati Saudi Arabia inapinga tabia hiyo.

Waandamanji wa Iran walishambulia ubalozi wa Saudia mjini Tehran, na kuwasha baadhi ya jingo lake moto, baada ya Saudi Arabia ilipomuuwa kiongozi wa kishia msaudia, Sheik Nimr al Nimr pamoja na wenzake 46.

Rais wa Iran Hassan Rouhani wiki ilopita alilieleza shambulizi la ubalozi wa Saudi Arabia, kuwa ni kosa na ni kinyume cha sharia. Lakini anasema Saudi Arabia haiwezi kutumia kisingiuzio cha kuvunja uhusiano wa kibalozi na Iran, ili kuficha uhalifu wake wa kumuuwa sheik al Nimr aliyekua mkosowaji wa ufalme wa Saudi.

Mkuu wa Umoja wan chi za kiarabu Nabil al Arabi, amehimiza Iran kupunguza mivutano na majirani zake kwa kuchukuwa hatua thabiti.

Bw Al Arabi anasema inaiangukia Iran kuchukuwa hatuwa madhubuti za kuthibitisha nia yake ya kuimarisha uhusiano na majirani zake wa kiarabu na kupunguza hofu za kuingilia kati masuala yao ya ndani.

Profesa wa sayansi ya kisiasa kwenye chuo kikuu cha American University mjini Beirut, Hilal Khashan ameiambia sauti ya America kuwa hadhani kuwa mkutano wa umoja wa nchi za kiaabu utapelekea hatuwa zozote thabiti.

Khasan anaongeza anasema Iran imekariri tena kuwa haina haja ya kuzidisha uhasama na Saudi Arabia, na kwamba imewasimamisha kazi baadhi ya maafisa wa polisi kutokana na shambulizi la ubalozi wa Saudi.

XS
SM
MD
LG