Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 08:06

Salva Kiir kutia saini mkataba wa Amani, Juba


Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na mpinzani wake Riek Machar, walipokutana uso kwa uso mjini Addis Ababa, Jan. 29, 2014.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) na mpinzani wake Riek Machar, walipokutana uso kwa uso mjini Addis Ababa, Jan. 29, 2014.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir alikutana na viongozi wa kikanda Jumatano kabla ya kutia saini makubaliano ya amani na waasi huku kukiwa na vitisho vya vikwazo vya Umoja wa Mataifa ikiwa atashindwa kukubaliana na mpango huo.

Msemaji wa Rais, Ateny Wek Ateny, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba, bwana Kiir atasaini makubaliano ya amani lakini serikali imesema bado kuna masuala ya kujadiliwa katika baadhi ya sehemu juu ya suala la kushirikiana madaraka.

Mpaka sasa angalau kumeshafikiwa makubaliano saba ya kusimamisha mapigano na kuvunjwa ndani ya siku kadhaa katika taifa changa kabisa duniani ambalo lilijitenga kutoka Sudan mwaka 2011.

Mkataba wa hivi sasa utawapatia waasi nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais ikimaanisha kwamba mkuu wa waasi bwana Riek Machar ana uwezekano mkubwa wa kurejea kwenye wadhifa ambao alifukuzwa hapo Julai mwaka 2013, miezi sita kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuanza.

Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini, Riek Machar
Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini, Riek Machar

Bwana Machar tayari alishatia saini mkataba hapo Agosti 17 lakini kwa wakati huo Rais Kiir alikubaliana na maelezo kadhaa. Serikali yake kisha iliiushutumu mkataba huo ukisema kuwa haufai na alisema alihitaji muda zaidi kwa mashauriano.

Waasi walidai mapigano yaliendelea Jumatano katika maeneo kadhaa.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hapo Jumanne liliongeza shinikizo kwa Rais Kiir kuunga mkono mkataba wakimuonya walikuwa tayari kuchukua hatua haraka kama bwana Kiir hatofanya hivyo.

XS
SM
MD
LG