Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:01

Rwanda yakutana na uongozi wa mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda-ICTR.


Rais wa Paul Kagame wa Rwanda.
Rais wa Paul Kagame wa Rwanda.

Serikali ya Rwanda na mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda (ICTR) iliyoko Arusha zimekukubaliana kwamba kuna mambo ambayo pande hizo mbili zinaona hayaku kamilika wakati mahakama hiyo itakapomaliza kazi zake mwezi Disemba mwaka huu.

Ujumbe wa mahakama hiyo unaoongozwa na Rais wakeVagn Prusse Joensen akiwa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Abubakar Jallow wamekua na mazungumzo na maafisa wa juu wa sheria nchini Rwanda.

Katika miaka 20 ya kazi za mahakama hiyo, iliyoendesha kesi za wahusika wa mauaji ya halaiki ya Rwanda, kumekuwepo na malalamiko kwamba mahakama hiyo haijafanya vya kutosha kuendesha kesi za washukiwa kwa kiwango kilichotegemewa na Rwanda. Lakini waziri wa sheria wa Rwanda na mwanasheria mkuu wa nchi hiyo Johnston Busingye alhamisi walijizuia kulaumu moja kwa moja .

“Leo hatujaja hapa kulaumu wala kupima mafanikio au kushindwa kwa mahakama hiyo lakini tunafahamu kwamba mahakama hii iliongozwa na watu kwa ajili ya kuhudumia maslahi ya watu wengine na hii ina maana hata wao kuna sehemu wanahisi hawakutekeleza vema majukumu yao. Suala la msingi leo ni kuagana na kutazama hatua inayofuata.”alisema Johnston Busingye.

Kwa upande wake rais wa mahakama hiyo Joensen amesema, ingawa hakufafanua zaidi kua mfumo wa mahakama za Ufaransa ndiyo imekuwa ikinyooshewa kidole na Rwanda kwa kutotoa ushirikiano katika kuwakamata washukiwa wa mauaji ya Rwanda walioko bado katika nchi hiyo ya Ulaya.

“Tulipopeleka shitaka hili kwa serikali ya Ufaransa tulidhani mahakama za Ufaransa zingendeesha kesi hii na mshukiwa kukutwa na hatia kwa sababu tulitoa ushahidi wa kutosha, kuhusu nafasi ya mtu huyo lakini hawakufanya hivyo kwa sababu mahakama zao ni huru. Na kuamua kufanya sisi kama ICTR hatukuwa na nafasi yoyote katika hilo.” alisema Vagn Prusse Joensen.

Mpaka sasa ni mtu mmoja tu ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela nchini Ufaransa kutokana na jukumu lake kwenye mauaji ya Rwanda, na mwezi uliopita mahakama ya rufaa ya Ufaransa iliamua kuacha kumfuatilia kisheria, kasisi mmoja wa kanisa katoliki Wenceslas Munyeshyaka ambaye kwa muda kesi yake kuhusu mauaji ya Rwanda imekuwa ikiendelea huko Ufaransa.

Mahakama ya ICTR inatazamiwa kukamilisha shughuli zake mwezi ujao wa Desemba baada ya kuwatia mbaroni washukiwa 93 wa mauaji ya halaiki ya Rwanda huku ikiamua kutupilia mbali kesi za washukiwa 61 tu.

Hilo ndilo jambo ambalo Rwanda imekuwa ikinyoosha kidole cha kutoridhishwa na mwenendo huo wa mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda- ICTR.

XS
SM
MD
LG