Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:37

Kuapishwa kwa Trump ni fursa na changamoto kwa Marekani


Rais mteule Trump
Rais mteule Trump

Kihistoria kuaapishwa kwa marais Wamarekani kumekuwa ni kielelezo cha kukabidhiana madaraka kwa amani na mara nyingi kunaonyesha mabadiliko ya kisiasa.

Mwandishi VOAJim Malone anatusimulia kuwa hiyo ni desturi ya demokrasia ya Marekani inayorudi miaka mingi nyuma kama taifa lenyewe.

Amesema kuapishwa kwa rais mpya ni kiashiria cha kumalizika kwa ungwe moja kwenda ungwe nyengine, katika hali zote wakati wa raha na wakati wa shida.

Roosevelt

Mnamo mwaka 1933, Franklin Roosevelt aliapishwa wakati taifa likikabiliwa na hali mbaya ya uchumi.

Rais Roosevelt ambaye ni rais wa 32 aliliambia taifa kuwa: “Kwanza kabisa, napenda kuweka wazi imani yangu isiyo na shaka kwamba kitu ambacho tunatakiwa kukiogopa ni uwoga wenyewe.”

Kennedy

Mnamo mwaka 1961, John Kennedy alikuwa rais wa 35 aliwahamasisha vijana wa Marekani kwa kuhimiza jukumu la kujitolea.

FILE - Rais John F. Kennedy akihutubia taifa baada ya kuapishwa mwaka 1961.
FILE - Rais John F. Kennedy akihutubia taifa baada ya kuapishwa mwaka 1961.

“Kwa hivyo Wamarekani wenzangu, msiulize nini nchi yenu itawafanyia. Jiulizeni nini mnaweza kulifanyia taifa lenu.”

Reagan

Miaka ishirini baadae, Ronald Reagan wa Republikani rais wa 40 aliingia kwenye madaraka na ahadi za kupunguza ukubwa wa serikali.

“Katika hali hii iliyoiyumbisha taifa, serikali sio mtatuzi wa matatizo haya, bali serikali ndio tatizo lenyewe.”

Rais Ronald Reagan akiapishwa, January 21, 1985.
Rais Ronald Reagan akiapishwa, January 21, 1985.

Rais mteule Donald Trump anasema kwa kweli huu ni wakati wakufurahisha kuwa unaishi. Bado historia haijaandikwa. Hatujui namna ukurasa wa historia hiyo utavyosomeka kesho. Lakini kwa mara ya kwanza kwa miaka mingi tunachojua ni kuwa kurasa za historia hiyo zitatungwa na kila moja kati yenu. Huu ni msafara.”

Wasemavyo wachambuzi

Mchambuzi John Fortier anasema hata hivyo nchi imegawanyika baada ya Trump kushinda, na moja ya changamoto mpya inayomkabili rais ni kuleta umoja.

Mchambuzi huyo kutoka Kituo cha Sera za Makubaliano amesema kuwa: Nafikiri ni fursa muhimu, kwa hatua ya kwanza kwa kweli rais kulihutubia taifa, kuwaambia sasa kama rais kuwa pengine baadhi ya tofauti zilizojitokeza kwenye kampeni tuziachilie mbali.

kihistoria, kuapishwa kwa rais ni wakati ambao mfukuto wa kampeni za kisiasa unatakiwa utupiliwe mbali kwa azma ya kuliendeleza taifa na demokrasia, amesema John Hudak.

Hudak ambaye yuko na Taasisi ya Brookings anasema: “Rais Obama atapanda gari pamoja na Rais mteule Trump kwenda kwenye viwanja vya Bunge la Marekani wakitokea White House na kwa utulivu kabisa atakabidhi madaraka na kumshuhudia mrithi wake, nasio yule aliyekuwa ni pendeleo lake, lakini bado ni mrithi aliyemkubali, ambaye ataapishwa rasmi. Jambo hili halitokei kila pahala duniani na ni tukio muhimu hapa nchini.”

Lakini Trump anajulikana kwa kauli zake za kukurupuka katika mikutano ya kisiasa na vipi itakuwa hotuba yake baada ya kuapishwa? Kwa kweli haitabiriki, anasema mchambuzi Norm Ornstein.

Onstein wa Taasisi ya American Enterprise anasema: “Hotuba ya Trump baada ya kuapishwa kwa kawaida inaandaliwa na kuandikwa mapema, na marais wanasoma hiyo hotuba. Je Donald Trump atatupa hiyo hotuba iliyo andikwa na kusema yale anayoyataka nje ya hotuba? Itakuwa tuko nje ya utaratibu hapa.”

Lakini mwandishi wa VOA anasema kwa kuwa Trump ndio yuko kwenye hatua za mwisho kuwa rais wa 45, na kauli atayoitoa mwanzoni mwa kuchukua madaraka itatoa fununu jinsi ambavyo anataka awe ni kiongozi wa namna gani.

XS
SM
MD
LG