Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:11

Usalama na kuiunganisha Somalia ni kipaumbele changu: Rais Mohamud


Viongozi wa kigeni walohudhuria sherehe za kuapishwa rais mpya wa Somalia Hassan Sheihk Mohamud
Viongozi wa kigeni walohudhuria sherehe za kuapishwa rais mpya wa Somalia Hassan Sheihk Mohamud
Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametoa wito wa kukomeshwa ugaidi na uharamia katika taifa lake lililoharibiwa na vita alipokuwa anakula kiapo Jumapili mjini Mogadishu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Somalia kushuhudia sherehe za kuapishwa kwa rais mbele ya viongozi wa kigeni wanadiplomasia na wasomali mjini Mogadishu katika muda wa miaka 47.

Mara ya mwisho kwa sherehe kama hizo kufanyika ilikuwa rais wa kwanza wa Somalia Aden Abdulle Osman alipomkabidhi madaraka waziri mkuu Abdirashid Ali Sharmarke mwaka 1967, baada ya kupata ushindi katika uchaguzi wa rais. Sharmarke aliuliwa na kupinduliwa na Siad Barre mwaka1969.

Miongoni mwa viongozi walohudhuria sherehe za Jumapili zilizofanyika chini ya ulinzi mkali walikuwa, kiongozi wa Ethiopia Hailemariam Desalegn na rais wa Djibuti Ismail Omar Guelleh, makamu waziri mkuu wa Uturuki, na wawakilishi kutoka Sudan, Uganda, Qatar na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa.


Hatua hiyo imefikiwa kufuatia mpamgo ulosimamiwa na mataifa ya kanda ya Pembe ya Afrika na Umoja wa Mataifa katika juhudi za kumaliza vita vya karibu miongo miwili vilivyosababisha vifo vya maelfu na maelfu ya Wasomali.

Katika hotuba yake rais Mohamud alialihidi kuleta muelekeo mpya wa sera kwa misingi iliyowasi aliyoeleza kuwa ni “nguzo za mwanzo mpya kwa Somalia”.

"Moja kati ya hatua hizi ni kudumisha usalama na Somalia kuwa nchi inayowtawaliwa chini ya utawala wa sheria. Kipau mbele cha kwanza, cha pili na cha tatu ni kupatikana kwa usalama,” alisema rais Mohamud

Rais Mohamud anasema anataka Somalia ibaki kuwa taifa moja lililoungana, akitaka Somalia ya kusini iliyokuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Utaliana kuungana na Somaliland ya Ksakazini iliyokuwa chini ya utawala wa Uingereza.

Amesema ataendelea na mazungumzo yaliyokwisha anza kati ya pande hizo mbili. Anasisitiza kwamba anataka kufuata sera ya kuleta umoja kwa diplomasia na wala si kwa nguvu za kijeshi.

Sherehe hizi zimefanyika siku chacjhe tu baada ya rais mpya kunusurika kutokana na shambulio la bomu katika hoteli aliyokuwa anaishi nah ii leo amehama rasmi ikulu ya Mogadishu.
XS
SM
MD
LG