Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 02:40

Rais wa Somalia: Nchi haiko salama kufanya uchaguzi


Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud na mwenzake wa Uturuki (L), Recep Tayyip Erdogan walipokutana mwanzoni mwa mwaka huu mjini Mogadishu
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud na mwenzake wa Uturuki (L), Recep Tayyip Erdogan walipokutana mwanzoni mwa mwaka huu mjini Mogadishu

Rais wa Somalia aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba serikali yake haitafanya uchaguzi mkuu mwaka ujao kutokana na kuendelea kuwepo hali ya ukosefu wa usalama nchini humo.

Katika mahojiano Jumatano na VOA, Rais Hassan Sheikh Mohamud alisema kwamba uchaguzi wa “mtu mmoja, kura moja” hautawezekana kwa mazingira yaliopo hivi sasa.

Aliongeza kwamba upigaji kura unapotokea huwenda ukachukua mtizamo tofauti. “ni kanuni ya kidemokrasia kwamba kila mtu anastahili kupiga kura ya kumchagua anayemtaka, lakini kuna mwanya mkubwa kati ya pale na mahala tunaposimama”, Rais Mohamud alisema. “hatujawahi kusema uchaguzi hauwezekani kufanyika. Kuna hatua tofauti na mifano tofauti kwa uchaguzi na tuna lengo la kupata njia bora mbadala, lakini bado hatujakubaliana juu ya muundo wa mpito kwa mwaka 2016”.

Rais wa Somali, Hassan Sheikh Mohamud
Rais wa Somali, Hassan Sheikh Mohamud

Bwana Mohamud alikanusha kwamba jambo hilo litaonekana kama kushindwa kwa serikali yake kuheshimu ahadi walizotoa. “Hatujawahi kumuahidi mtu mmoja, kura moja na kuweka masanduku ya kupiga kura katika kila kituo nchini, aliiambia VOA. Tuliahidi utaratibu bora kuliko ule ambao umetuweka sisi madarakani, utaratibu rahisi na wenye kutambulika”.

Serikali ya sasa ilipewa mamlaka ya kuiongoza Somalia kuelekea uchaguzi mkuu kufuatia kuchaguliwa Rais Mohamud, bunge jipya na kupitishwa katiba mpya ya mwaka 2012.

Hata hivyo wanamgambo wa kundi la Al-Shabaab wanaendelea kufanya mashambulizi ya ghasia. Kundi hilo limeuwa wabunge kadhaa, lilifanya mashambulizi mawili kwenye makazi ya rais mwaka jana na bomu moja lililotegwa kwenye gari katika hoteli moja mashuhuri ya Mogadishu hapo Jumapili ambapo lilisababisha vifo vya watu 18.

XS
SM
MD
LG