Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:20

Rais wa Nigeria atangaza hali ya dharura


Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (katikati)
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (katikati)

Majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa kaskazini mashariki mwa Nigeria yamo chini ya ulinzi mkali.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya dharura katika majimbo matatu ya kaskazini mashariki kufuatia wimbi kubwa la ghasia linalohusiana na wanamgambo wa kiislamu.

Katika hotuba yake kwenye televisheni ya taifa Jumanne,bwana Jonathan alisema anapeleka vikosi zaidi kwenye majimbo ya Borno, Yobe, na Adamawa kwa kile alichokiita operesheni za ndani za usalama.

Kiongozi huyo wa Nigeria amesema majeshi yameamriwa kuchukua hatua zote muhimu kuzuia uasi na ugaidi na kuwa na mamlaka ya kukamata na kuchukua udhibiti wa jengo linalotumika kwa malengo ya kigaidi. Bwana Jonathan alikatisha ziara yake ya kusini mwa Afrika wiki iliyopita ili kushughulikia ghasia zinazoendeela nchini mwake.
XS
SM
MD
LG