Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:45

Rais wa Mali ashambuliwa na waandamanaji


Rais wa muda wa Mali Diouncounda Traore (katikati) akizungumza na kiongozi wa baraza la kijeshi Amadou Haya Sanogo (Kushoto) kwenye kambi ya jeshi.
Rais wa muda wa Mali Diouncounda Traore (katikati) akizungumza na kiongozi wa baraza la kijeshi Amadou Haya Sanogo (Kushoto) kwenye kambi ya jeshi.

Rais wa muda Dioncuounda Traore alichukuliwa katika gari la kubeba wagonjwa baada ya shambulizi.

Rais wa muda wa Mali amekimbizwa hospitali baada ya kushambuliwa na waandamanaji waliovamia ikulu ya rais .

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Anne Look katika mji mkuu Bamako, anaripoti kwamba rais wa muda Dioncuounda Traore alichukuliwa katika gari la kubeba wagonjwa baada ya shambulizi la Jumatatu.

Aliongea na mkuu wa utawala Souleymane Niafo ambaye amesema maisha ya Bw.Taraore hayako hatarini tena , lakini anatibiwa kwa majeraha. Majeraha ya Bw.Traore hayajulikani.

Tukio hilo lilitokea siku moja baada ya jumuiya ya kikanda ECOWAS na baraza la kijeshi kufikia makubaliano yatakayomruhusu Bw.Traore kubaki madarakani baada ya Jumanne pale mamlaka yake ya muda yalipokuwa yanamalizika.

Mkuu wa utawala anasema waandamanaji walikwenda Ikulu Jumatatu na kumtaka rais huyo wa muda aachie madaraka. Amesema baadaye waandamanaji hao walipambana na walinzi na kulazimisha kuingia ndani ya jumba la rais kwenye ofisi ya Bw.Traore ambako walimshambulia.

Amesema baadaye maafisa walifanikiwa kuwaondoa waandamanaji nje ya jumba la Ikulu.

XS
SM
MD
LG