Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:46

Rais wa Malawi ashutumiwa kwa ghasia


Rais wa Malawi Bingu Wa Mutharika
Rais wa Malawi Bingu Wa Mutharika

Mapema mwezi huu rais Mutharika alisema wafuasi wake hawana budi kuinuka na kumtetea baba yao kufuatia unyanyasaji kutoka kwa watoaji wa misaada wa kimataifa

Kiongozi mwandamaizi wa upinzani huko Malawi amemshutumu rais Bingu Wa Mutharika kwa kuchochea ghasia baada ya kuwashawishi wafuasi wake kumtetea katika mashambulizi ya kisiasa.

Mapema mwezi huu rais Mutharika alisema wafuasi wake hawana budi kuinuka na kumtetea baba yao kufuatia unyanyasaji kutoka kwa watoaji wa misaada wa kimataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu ambao aliwashutumu kwa kusababisha ghasia.

Lakini Humphrey Mvula makamu wa rais wa chama cha United Democratic Front ameimabia sauti ya amerika kwamba maelezo ya rais hayakuwa na msingi akisema kuwa rais anatakiwa kulaumiwa kama nchi itatumbukia katika mzozo wa kisiasa.

Rais Mutharika amekabiliwa na shinikizo la kutatua mzozo na wachangiaji wa kimataifa ambao wengi walisitisha msaada katika taifa hilo la kusini mwa afrika kufuatia maandamano ya kuipinga serikali yaliyokuwa na maafa makubwa.

XS
SM
MD
LG