Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 02:54

Rais wa Korea Kusini akubali kujiuzulu lakini kwa masharti


Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ainama kwa heshima alipokuwa akilihutubia taifa mjini Seoul, Nov. 29, 2016.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye ainama kwa heshima alipokuwa akilihutubia taifa mjini Seoul, Nov. 29, 2016.

Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye, amesema kuwa yuko tayari kuondoka madarakani iwapo bunge litapitisha kuwa afenye hivyo. Lakini rais huyo alisema atafanya hivyo kwa masharti fulani.

Akihutubia taifa kupitia televisheni siku ya Jumanne, Geun-hye alisema kuwa atasitisha mipango yake ya awali iwapo bunge litamtaka kufanya hivyo.

Hotuba yake ilitayarishwa kwa haraka.

Lakini punde tu baada ya hotuba hiyo, baadhi ya viongozi wa upinzani walielezea shaka yao kuhusiana na hatua ya rais huyo. Wengine walishuku kuwa alichukua hatua hiyo kama mbinu za kujiepusha na kura ya kutokuwa na imani na uongozi wake ambayo imewasilishwa kwenye bunge, na vile vile kupata wakati wa kutosha kutafuta wabunge kumunga mkono.

Choo Mi-ae, kiongozi wa chama cha Demikratik cha Korea, alisema kuwa hatua hiyo ya kutaka kujiuzulu kwa masharti haitasitisha mipango ya upinzani ya kuwasilisha mswada wa pamoja ambao ulitarajiwa kupigiwa kura siku ya Ijumaa.

Wiki moja kabla ya hapo, rais huyo alitajwa na kiongozi wa mashtaka kama mshukiwa katika kesi ya ufisadi, hali ambayo ilipelekea maandamano makubwa kwenye barabara za mji wa Seoul.

Siku ya Jumanne, Guen-hye aliomba msamaha kwa mara ya tatu mtwalia na kusema kuwa hakujua kama wandani wake walikuwa wanahusika katika visa vya usfisadi.

XS
SM
MD
LG