Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:30

Wanasiasa waliofungwa na rais Jameh wa Gambia waachiliwa


Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow
Rais mteule wa Gambia, Adama Barrow

Mwanasiasa mmoja maarufu wa upinzani nchini Gambia, pamoja na wengine kumi na wanane waliofungwa jela wakati wa utawala wa rais anayeondoka, Yahyah Jammeh, waliachiliwa huru Jumanne kufuatia ushindi wa Adama Barrow, kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika wiki jana.

Kundi la kutetea haki za binadam Amnesty International lilipongeza hatua hiyo, lakini kuonya juu ya kutowasahau wafungwa wengine waliowekwa ndani kwa ajili ya kutoa maoni yao.

Na huku wengi wakiendelea kusherehekea ushindi wa Barrow nchini kote, rais mteule ameapa kuwaachilia wafungwa Zaidi, na kwamba nchi hiyo haitajiondoa kutoka mahakama ya uhalifu ya kimataifa, ICC.

Rais Jammeh, ambaye ameongoza nchi hiyo kwa miaka ishirini na miwili, alishindwa na Adama Barrow, aliyeungwa mkono wa muungano wa vyama vya upinzani. Baada ya ushindi wake, Barrow alisema kuwa hakuna mtu aliyedhani wakati kama huo ungefika.

XS
SM
MD
LG