Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:16

Rais wa Brazil kupigiwa kura leo iwapo kesi ya kumshitaki ianze au la


Rais wa Brazil, Dilma Rousseff
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff

Baraza la seneti la Brazil Jumanne litaanza kupiga kura iwapo au la kuanza kesi ya kumshtaki ili kumuondoa madarakani Rais Dilma Rousseff aliyekumbwa na matatizo ambapo huenda atakabidhi rasmi madaraka kwa makamu rais wake wa zamani, ambaye hivi sasa ni kaimu Michel Temer.

Licha ya kubashiri kwamba mjadala utaweza kuendelea hadi Jumatatno asubuhi inaonekana kuna uwezekano kwamba baraza la seneti litapiga kura kumshtaki rais huyo mwenye msimamo wa mrengo wa kushoto kwa vile wingi mdogo unahitajika wa maseneta .

Baraza la seneti lilimsimamisha kwa muda Rousseff mwezi Mei baada ya shutuma kuibuka kwamba kinyume cha sheria alibadili bajeti ya nchi na kuonesha kwamba uchumi wa nchi sio mbaya kama ambavyo ulivyokuwa wakati wa kampeni zake za kuchaguliwa tena mwaka 2014.

Katika utaratibu wote wa kumfungulia mashtaka Rousseff ameendelea kusema kwamba hakufanya jambo lolote baya na aliliita suala hilo ni mapinduzi ya kisiasa.

XS
SM
MD
LG