Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:22

Rais wa Brazili aliye mashakani aapa kupambana


Rais Dilma Rousseff akiwa na makamu wake Vice President Michel Temer kushoto.
Rais Dilma Rousseff akiwa na makamu wake Vice President Michel Temer kushoto.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff ameapa kuendeleza mapambano ya uwezekano wa kuondolewa madarakani.

Hatua hiyo inafuatia baada ya bunge la chini kupiga kura Jumapili usiku ya kumshitaki kwa shutuma za rushwa katika baraza la seneti.

Rais Roussef amesema hayo katika mkutano na wanahabari ambao ulirushwa moja kwa moja na televisheni na kusema ni kitu kisicho kubalika.

Amesema kwamba ana ari, uchu na kutotishika na kamwe hawezi kushindwa ama kurudi nyuma.

Amendelea kusema huo ni mwanzo wa mapambano ambayo yatakuwa makubwa na ya kukumbukwa.

Rais Rousseff alitoa maneno makali kwa makamu wa Rais Michel Temer, mshirika wake wa kisiasa wa zamani.

Makamu huyo wa rais ni kiongozi wa mchakato huo na atakuwa kiongozi wa nchi endapo Rais huyo ataondolewa madarakani.

Alimwita makamu huyo wa rais msaliti.

XS
SM
MD
LG