Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 18:04

Marekani na GCC jinsi ya kupambana na ISIL


Rais wa Marekani Barack Obama akishirikikatika mkutano wa Gulf Cooperation Council (GCC) mjini Riyadh, Saudi Arabia April 21, 2016.
Rais wa Marekani Barack Obama akishirikikatika mkutano wa Gulf Cooperation Council (GCC) mjini Riyadh, Saudi Arabia April 21, 2016.

Rais wa Marekani Barack Obama na viongozi wa ghuba bado wameungana katika juhudi za kuliharibu kundi la Islamic Sate na kuleta uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati lililokumbwa na mzozo.

"Bado tumeungana katika mapambano ya kulivunja ISIL, ambalo ni tishio kwetu sote," amesema Obama akiwa mjini Riyadhi na kusema kuwa wanahcama wa baraza la ushirikiano wa ghuba GCC pia wataendelea "kuongeza michango yao katika mapambano dhidi ya ISIL.".

Akiongea wakati wa kufunga kwa mkutano wa Alhamisi uliojumuisha mataifa sita wanachama wa GCC, rais amerejea kuelezea nia ya dhati ya Marekani, kuwa "haitatetereka na itakabiliana na kundi hilo kwa nguvu zote."

Marekani na GCC wamekubaliana pia kwamba suluhisho la kisiasa linahitajika nchini Syria. Obama amesema wamekubaliana kwamba njia pekee kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ni kupitia serikali ya mpito na kuondoakna na Rais Bashar al-Assad.

XS
SM
MD
LG