Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:27

Rais Obama aonya viongozi Sudan kusimamisha operesheni za kijeshi.


Rais Barack Obama .
Rais Barack Obama .

Rais Obama atoa onyo kwa viongozi wa Sudan na kuwataka kukamilisha wajibu wao kwa kumaliza ghasia.

Rais wa Marekani Barack Obama ameitaka serikali ya Sudan kusimamisha kabisa operesheni zake za kijeshi katika eneo la kusini la sivyo itatengwa na jamii ya kutengwa kimataifa.

Katika taarifa iliyorekodiwa , Bw.Obama amesema serikali ya Sudan lazima iache mara moja operesheni za kijeshi Kordofan Kusini ikiwa pamoja na mashambulizi ya anga na kusababisha raia kupoteza makazi yao.

Bw. Obama alichukua hatua isiyo ya kawaida ya kurekodi ujumbe wa sauti Jumanne jioni , uliolenga viongozi wa Sudan mara tu baada ya kurudi kutoka kwenye matembezi kwenye eneo la himaya ya Marekani la Puerto Rico.

Amesema viongozi wa pande zote Sudan Kusini na Kaskazini sharti wakamilishe wajibu wao na kukubaliana kumaliza ghasia .

Sudan Kusini inajiandaa kwa sherehe za kutangaza rasmi uhuru wake Julai 9, na kuwa taifa jipya kabisa duniani.

XS
SM
MD
LG