Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:50

Rais Obama ahimiza mageuzi Mashariki ya Kati


Rais Barack Obama akitoa hotuba juu ya Mashariki ya Kati akiwa wizara ya mambo ya nje mjini Washington.
Rais Barack Obama akitoa hotuba juu ya Mashariki ya Kati akiwa wizara ya mambo ya nje mjini Washington.

Amani ya kudumu ni jambo linalohitajika kwa haraka sana kuliko wakati wowte ule kati ya Isrtael na Palestina alisema rais Obama.

Akizungumza kutoka wizara ya mambo ya nchi za nje siku ya Alhamisi, rais wa Marekani alipongeza "mabadiliko ya kipee" yanayotokea Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, lakini alisema nchi nyingi zimejibu wito wa mageuzi kwa utumiaji nguvu.

Rais Obama alisema mfano wa kipekee ni Libya, ambako anasema Moammar Gadhafi ameanzisha vita dhidi ya raia wake. Anasema maelfu ya watu wengeli uliwa ikiwa Marekani na washirika wake hawakuchukua hatua.

Alisema Syria pia imechagua "njia ya mauwaji na kukamatwa haliaki ya watu." Bw Obama alitoa wito kwa rais wa Syria Bashar al-Assad kuongoza kipindi cha mpito kuelekea demokrasia au "kuondoka njiani."

Akizungumzia matukio ya Misri na Tunisia Bw.Obama alitaja kwamba mnamo miezi sita iliyopita viongozi wawili wameacha madaraka na kusema kuna mengi zaidi yatakayofuatia wakati wananchi wanasimama na kudai haki zao za msingi.

Amani ya Mashariki ya Kati

Rais Obama amesema, amani ya kudumu ni muhimu kufikiwa sasa kulko wakati wowote ule kati ya Waisreal na Wapalestina. Alitoa wito wa kuundwa kwa mataifa mawili, kuidhinisha ombi kuu la Wapalestina kwamba mipaka ya taifa lao liundwe kufuatana na mipaka ya 1967.

Alikiri kwamba kushiriki kwa kundi la Hamas linaloungwa mkono na Iran katika serikali ya Palestina kuna zusha masuala muhimu ya haki kutoka kwa Israel, ikiwa ni pamoja na swali kwamba vipi majadiliano yanaweza kufanyika na kundi ambalo linakata kutambua haki ya Israel kuwa taifa. Alisema viongozi wa Palestina wanabidi kutoa jibu la kuaminika kwa swali hillo.

XS
SM
MD
LG