Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 11:30

Rais Obama aanza ziara ya Afrika


Rais Barack Obama akizungumza katika bunge la Ghana mjini Accra, 11 Julai 2009
Rais Barack Obama akizungumza katika bunge la Ghana mjini Accra, 11 Julai 2009

Rais Barack Obama anafanya ziara ya pili barani Afrika kuanzia leo Jumatano. Atazuru Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.

Rais wa Marekani Barack Obama Jumatano anaanza ziara ya wiki moja nzima katika nchi tatu za Afrika kwa lengo la kuhamasisha demokrasia na uwekezaji wa Marekani barani humo.

Rais Obama atakwenda Senegal leo Jumatano ambako atakutana na rais Macky Sall na kesho Alhamis atatembelea nyumba ya kihistoria ya watumwa wa Afrika walioletwa Marekani katika kisiwa cha Goree.

Ijumaa bwana Obama atakwenda Afrika Kusini ambako atakutana na rais Jacob Zuma na kutembelea kisiwa cha Robben ambacho rais wa zamani Nelson Mandela alifungwa jela.

Maafisa wa Afrika Kusini walisema ziara ya bwana Obama itaendelea licha ya kuwepo na hofu kote nchi humo kuhusu kudhoofika kwa afya ya bwana Mandela. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini mwenye miaka 94 yuko katika hali mahtuti na amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
XS
SM
MD
LG