Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:43

Rais Mutharika wa Malawi yuhali mahututi


Rais Bingu Wa Mutharika wa Malawi akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa viongozi wa AU mjini Kampala. Uganda July 27, 2010)
Rais Bingu Wa Mutharika wa Malawi akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa viongozi wa AU mjini Kampala. Uganda July 27, 2010)

Rais Bingu wa Mutharika amesafirishwa usiku wa manane Alhamisi hadi Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kupata mshituko wa moyo.

Vyombo vya habari vya Malawi vinaeleza kwamba Rais Mutharika amesafirishwa hadi Johanesburg, Afrika Kusini kwa matibabu akifuatana na mkewe na jamaa wa karibu na rais huyo.

Alipelekwa kwa haraka katika hospitali kuu mjini Lilongwe katika mji mkuu wa Lilongwe, baada ya kuripotiwa amepata mshtuko wa moyo na amepoteza fahamu.

Serikali haikutangaza ugonjwa wake, lakini vyanzo vya kidiplomasia vinaeleza kwamba kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 78 alikua na matatizo ya moyo, na alianguka jana akiwa ikulu na kupoteza fahamu.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Makamu wa Rais Bi. Joyce Banda aliwaomba wa-Malawi kumombea kiongozi wao na kuwa pamoja, kumombea apate afueni, lakini hakutoa maelezo juu ya ugonjwa wake.

Bw Mutharika alichaguliwa rais mara ya kwanza 2004 na kushinda uchaguzi wa mhula wa pili 2009. Wakosowaji wa rais wanasema amezidi kuwa kiongozi wa kimabavu tangu kushinda mhula wa pili.

Chini ya katiba ya Malawi Makamu wa Rais Bi. Banda anatarajiwa kukamilisha miaka miwili iliyobaki ya mhula ya Bw. Mutharika ikiwa hatoweza kuendelea na kazi tena.

XS
SM
MD
LG