Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:01

Barabara yapatiwa jina la Rais Kibaki mjini Dar es Salaam


Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais Mwai Kibaki wa Kenya
Rais wa Kenya Mwai Kibaki amefanya ziara nchini Tanzania ambayo ametumia kama njia ya kutoa mkono wa kwaheri wakati huu ambapo kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu machi 4 mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Moja ya kumbukumbu kubwa aliyopata katika ziara yake ya kuwaaga watanzania waliopo jijini Dar Es Salaam ni kupewa jina lake katika moja ya barabara maarufu iliyokuwa ikijulikana kama Old Bagamoyo Road na sasa inaitwa “MWAI KIBAKI ROAD".

Rais Kibaki akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete alizindua barabara hiyo Alhamis yenye jina la barabara ya Mwai Kibaki.

Barabara hii kwa mujibu wa meya wa manispaa ya Kinondoni Rajab Mwenda ina historia ya kuwa imepita katika makazi ya marais wote wa Tanzania tangu muasisi wa taifa la Tanzania hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere hadi Rais wa sasa Jakaya Kikwete.

Shughuli nyingine iliyofanyika katika ziara ya Rais Kibaki nchini Tanzania ni mazungumzo aliyoyafanya Rasi huyo wa Kenya na wazee wa mkoa wa Dar Es Salaam ambapo Rais Kibaki alisisitiza kuimarisha ushirikianao wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili ili kuchochea kasi ya maendeleo katika ukanda huu wa Afrika mashariki.

Kenya na Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umeimarishwa zaidi hivi sasa katika mtengamano ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC.
XS
SM
MD
LG