Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 13:06

Rais Jonathan asema tena "wasichana watakombolewa"


Jamii ikishikilia mabango yanayosema "Rudisha wasichana wetu" baada ya Boko Haram kuwateka wasichana wa shule nchini Nigeria
Jamii ikishikilia mabango yanayosema "Rudisha wasichana wetu" baada ya Boko Haram kuwateka wasichana wa shule nchini Nigeria
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anasema serikali yake itaendelea kufanya kila iwezalo kuwarudisha nyumbani zaidi ya wasichana wa shule 200 ambao walitekwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram mwezi uliopita.

Katika hotuba iliyorekodiwa na kutolewa hadharani Alhamis, Rais Jonathan alieleza kwamba ni siku 45 tangu “utekaji wa kutisha” ufanyike dhidi ya wasichana hao.

Aliahidi kuendesha vita vikali dhidi ya ugaidi na alisema alitoa mwongozo kwa majeshi yake ya usalama kutumia njia zozote halali zinazostahili kumaliza kinga ya magaidi kwenye ardhi ya Nigeria.

Rais alitoa matamshi hayo kwenye hotuba inayoadhimisha siku ya demokrasia, ambayo ni sikukuu ya kitaifa nchini humo. Alisema serikali yake ilikuwa wazi kwa mashauriano na raia ambao waliunga mkono al-Qaida au makundi mengine kama hayo kama wanaacha ugaidi.

Jumatatu, ofisa mmoja wa jeshi wa cheo cha juu alisema jeshi linajua mahala walipo wasichana wanafunzi waliotekwa, lakini alisema itakuwa vigumu kutumia nguvu kuwaokoa wasichana hao.

Mkuu wa ulinzi, Alex Badeh aliwaambia waandishi wa habari mjini Abuja kwamba operesheni ya kijeshi itaweza kuwa hatari ili kuwaokoa wasichana hao. Alisema “hatuwezi kuwauwa wasichana wetu kwa ajili ya kujaribu kuwarudisha nyumbani”.
XS
SM
MD
LG