Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 16:18

Rais wa Chad atarajiwa kushinda uchaguzi Jumatatu


Rais wa Chad Idriss Deby akiwasalimia wafuasi wake wa Patriotic Salvation Movement wakati wa mkutano katika mji mkuu N'djamena
Rais wa Chad Idriss Deby akiwasalimia wafuasi wake wa Patriotic Salvation Movement wakati wa mkutano katika mji mkuu N'djamena

Wagombea watatu wa juu wanaompa changamoto Rais Deby wamesusia kushiriki upigaji kura wa Jumatatu.

Rais wa Chad Idris Deby anatarajiwa kushinda kipindi kingine cha uongozi katika uchaguzi wa rais ambao umesusiwa na wapinzani wake wakuu.

Uchaguzi umepangwa kufanyika Jumatatu baada ya kuakhirishwa mara tatu, lakini wapinzani watatu wa juu wa Bwana Deby wamejiondoa katika kinyang'anyiro, na kuwataka wapiga kura nao kususia uchaguzi. Viongozi wa upinzani wamekuwa wakidai mageuzi katika uchaguzi, ikiwa ni pamoja na orodha mpya ya wapiga na kadi za wapiga kura.

Wagombea wawili kutoka vyama vidogo vya upinzani bado wako katika ushindani, lakini Bwana Deby anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwashinda kwa idadi kubwa ya kura.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana Ijumaa, Bwana Deby amesema viongozi wa upinzani wamejiondoa kwasababu hawana fedha za kufanyia kampeni na walifahamu fika kuwa watashindwa. Amesema anatarajiwa kuwa idadi kubwa ya watu itajitokeza kupiga kura.

Wachambuzi wanasema watafuatilia kuona idadi ya wapiga kura watakaojitokeza Jumatatu kama hatua ambayo itaonyesha ni kwa kiasi gani wananchi wa Chad wamesikiliza maombi ya upinzani ya kususa.

vyama vya upinzani katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2006 vilisusia upigaji kura, wakati Bwana Deby alipochaguliwa tena. Walishiriki katika chaguzi za bunge mapema mwaka huu, ikiwa ni uchaguzi wa kwanza tangu mwaka 2002, lakini walidai kuwa chama cha Bwana Deby kilishinda kwa wizi.

Rais Deby ametawala Chad tangu akamate madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1990. Chini ya utawala wake, taifa limekuwa ni mzalishaji wa mafuta, lakini nchi bado imegubikwa na umaskini.

Anaendelea kukumbana na changamoto za waasi upande wa mashariki, ambao kwa muda mfupi waliuvamia mji mkuu mwaka 2008.

XS
SM
MD
LG