Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:12

Raila amuhakikishia ulinzi Gbagbo


Rais Laurent Gbagbo wakati alipolihutubia taifa na kusisitiza kuwa ni rais halali nchini humo, 21 Dec 2010
Rais Laurent Gbagbo wakati alipolihutubia taifa na kusisitiza kuwa ni rais halali nchini humo, 21 Dec 2010

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga anamuhakikishia ulinzi rais asiyekubalika kimataifa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, kama anakubali kujiuzulu. Waziri Mkuu huyo ambaye alichaguliwa na Umoja wa Afrika kuongoza juhudi za kutatua mgogoro wa kisiasa katika taifa hilo la Afrika Magharibi, alitoa matamshi hayo baada ya kukubali nafasi hiyo Jumatatu. Amesema atachukua nafasi hiyo ya Umoja wa Afrika kama ujumbe wa wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi- ECOWAS ambao unasafiri kwenda kukutana na bwana Gbagbo utashindwa kukubaliana nae.

Wakati huo huo kundi la marais wa nchi za Afrika Magharibi wanapanga kumweleza rais huyo wa Ivory Coast Laurent Gbagbo kuachia madaraka na kukubali matokeo ya uchaguzi yanayoonyesha mpinzani wake alishinda katika uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

Marais kutoka Sierra Leone, Cape verde na Benin waliwasili Abidjan Jumanne kuwasilisha wito kutoka ECOWAS, ambao umetishia kutumia nguvu kama bwana Gbagbo hataondoka madarakani.

Viongozi hawa wanakutana na bwana Gbagbo kumshawishi kumpa nafasi ya hifadhi ya kisiasa ikiwa ni moja ya taratibu za kubadilishana kutokana na kukubali kujiuzulu kwake. Pia watakutana na mpinzani wa bwana Gbagbo, Alassane Ouattara.

XS
SM
MD
LG