Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:05

Sikumkosea heshima Rais Kenyatta, asema Raila


Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema hakususia makusudi maadhimisho ya Madaraka Day mjini Nakuru, kufuatia mwaliko wa rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, na akaeleza kwamba mwaliko huo ulitolewa nyakati za mwisho mwisho.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema hakususia makusudi maadhimisho ya Madaraka Day mjini Nakuru, kufuatia mwaliko wa rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, na akaeleza kwamba mwaliko huo ulitolewa nyakati za mwisho mwisho.

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema hakususia kwa makusudi maadhimisho ya Madaraka Day mjini Nakuru, kufuatia mwaliko wa rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, na akaeleza kwamba mwaliko huo ulitolewa nyakati za mwisho mwisho.

Na BMJ Muriithi

Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya, Raila Odinga, amesema kwamba hakususia kwa makusudi maadhimisho ya mwaka huu ya Madaraka Day yaliyofanyika mjini Nakuru, kufuatia mwaliko wa rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, na akaeleza kwamba mwaliko huo ulitolewa nyakati za mwisho mwisho.

Kiongozi huyo wa muungano wa upinzani, CORD, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba yeye na wenzake walikuwa wamepanga kuhudhuria mkutano ulioidhinishwa na mahakama ya juu katika bustani ya Uhuru Park mjini Nairobi, na ingekuwa vigumu kubadilisha ratiba hiyo.

Aidha amesema kuwa alipokutana na rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne, walikubakliana kwamba pande mbili zinazozozana kuhusu uhalali wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini humo, zitatoa wabunge watano kila mmoja ili kutafuta suluhisho la mgogoro huo.

"Cord itatangaza majina ya wabunge na maseneta watano hapo kesho Alhamisi na tunataka Jubilee itangaze wake kufikia Ijumaa, iwapo wanataka tusitishe maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumatatu ya wiki kesho," alisema Odinga.

Awali, kwenye hotuba aliyoitoa katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru siku ya Jumatano, Bwana Kenyatta alieleza kutoridhika kwake na viongozi wa upinzani ambao alisema licha ya kuwaalika, hawakuhudhuria hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 53 tangu Kenya kupata Uhuru wa ndani.

"Sijui ni kwa nini hawakuhudhuria hafla hii na ili hali tuliwaalika.Ni lazima wajue ya kwamba wao pia wangependa kuheshimiwa iwapo watachukua uongozi," alisema Kenyatta.

Lakini Raila alisema hangebadilisha mipango ya awali ili kuhudhuria tamasha hizo.

"Sikunuia kumdharau rais hata kidogo kwa kutohudhuria maadhimisho hayo," alisema Odinga. "Ninafuraha kwamba mazungumzo kati ya pande zote mbili yalianza jana wakati tulipokutana na rais Kenyatta katika ikulu ya Nairobi. Nina matumaini kwamba tutaendelea kuzungumza na kutatua mzozo uliopo kwa sasa. Hakuna haja ya kwendelea kurushiana maneno," aliongeza Odinga.

Mwanasiasa huyo alizungumza na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu kutoka mjini Nairobi, Kenya. Sikiliza mahojiano yake hapa:

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:25 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG