Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:31

Prince William kuzungumza na Obama


Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakiwa na Prince William na mkewe Kate
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakiwa na Prince William na mkewe Kate

Prince William wa Uingereza anakutana Jumatatu na Rais wa Marekani Barack Obama huko White house. Mfalme huyo wa baadae anatarajiwa kuzungumza na Rais kuhusu biashara haramu ya wanyama pori.

Baada ya mkutano wake na bwana Obama, William atatoa hotuba kwenye mkutano wa Benki ya Dunia wa International Corruption Hunters Alliance mjini Washington.

Anatarajiwa kusema biashara haramu ya pembe za ndovu, pembe za faru na sehemu nyingine za mnyama ni “moja ya chanzo kikuu cha rushwa na uhalifu duniani hii leo” na wale wanaoangalia “njia nyingine au wanatumia mapato haramu kwa uhalifu huu lazima wawajibishwe”.

Prince William pia ataelezea kwamba baadhi ya viungo vya mnyama vina thamani kubwa zaidi ya uzito wao katika dhahabu.

Prince Harry (L) Kate (C) na Prince William (R) wakiwa Glasgow
Prince Harry (L) Kate (C) na Prince William (R) wakiwa Glasgow

William, mke wake Kate na kaka yake Prince Harry ni waanzilishi wa taasisi ya hisari ya Britains United for Wildlife.

Familia hiyo maarufu ya malkia wa Uingereza iliwasili New York, Marekani jumapili kwa ziara ya siku tatu nchini Marekani. Ni mara yao ya kwanza kwa familia hiyo kufika jiji la New York.

XS
SM
MD
LG