Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:49

Prince, gwiji wa muziki Marekani afariki dunia


Mwanamuziki maarufu wa Pop Marekani, Prince Rogers Nelson amefariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 57.

Kifo kimemkuta nyumbani kwake katika jimbo la Minnesota. kwa mujibu wa shirika la habari la AP.

Prince alilazwa hospitali wiki iliyopita baada ya ndege yake kutua kwa dharura huko Moline na alitoka hospitalini baada ya kutangazwa kuwa alikuwa na mafua makali.

Prince mmoja wa wasanii wakubwa wa muziki atakayekumbukwa sana ameishi miaka yote mji wa nyumbani kwao anakotokea wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota.

Atakumbukwa kwa nyimbo zake maarufu pamoja na albam zake ambapo ya kwanza ilitoka mwaka 1978 ya "For you," 1984 alitoa "Purple Rain" iliyotamba na kushika nambari moja katika chati za Billboard na pia kutoa filam iliyobeba jina hilo hilo.

Alabam yake ya mwisho na kampuni ya Warner Bros aliitoa 1996 "Chaos and Disorder."

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Ameshinda tuzo mbali mbali za Grammy na Oscar na alimshinda Michael Jackson 1985 kwenye American Music Awards, pia ameshirikiana na bendi mbali mbali ikiwa ni pamoja na Time , the New Power Generation na The Revolution.

XS
SM
MD
LG