Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:04

Maambukizo ya Malaria kwa wanawake wajawazito yapungua barani Afrika


Wanawake wakiwa wameshikilia vyandarua vilotiwa dawa ya kuzuia mbu
Wanawake wakiwa wameshikilia vyandarua vilotiwa dawa ya kuzuia mbu

Shirika la afya duniani limependekeza utafiti mkbwa zaidi kufanywa kutazama ufanisi wa dawa ya Dihydroartemisininpiperarquinine, kabla kuipendekeza katika kuzuia Malaria katika wanawake wajawazito.

Katika nchi zinazo kumbwa na ugonjwa wa Malaria barani Afrika, si jambo la ajabu kwa wanawake wajawazito kuambukizwa na mbu wanaobeba Malaria. Ugonjwa huo unawaweka watoto wachanga katika hatari ya kufariki. Lakini mkakati mpya wa uzuiwaji unatowa matumaini kuwa wanawake wajawazito wataweza kujifunguwa watoto wenye afya njema.

Hatari ya wanawake wajawazito kuathiriwa na Malaria iko juu sana katika nchi zinazoendelea barani Afrika. Watafiti wanasema asli mia 60 ya wanawake walojitokeza kushiriki katika utafiti wa kuzuia Malaria, walikuwa na vimelea.

Malaria inahusika na zaidi ya vifo laki moja vya watoto wachanga barani afrika kusini mwa jangwa la sahara kila mwaka. Ugonjwa huo unaweza pia kusababisha watoto kuzaliwa mapemaau wakizaliwa wakiwa na uzito mdogo, mambo yote ambayo ni hatari kwa kusababisha vifo vya watoto wachanga.

Kwa hiyo, wanawake wajawazito katika maeneo ambayo huathirika na Malaria, wanahimizwa kulala ndani ya vyandaruwa vilotiwa dawa ya mbu.

Wengi pia huwenda wakapewa mchanganyiko wa dawa yenye bei nafuu inayojulikana kama Sulfadoxinepyrimethamine, ambayo inapendekezwa na shirika la afya duniani ili kuwalinda dhidi ya Malaria.

Hio ndiyo ilikuwa tiba ya awali kwa ugonjwa huo, lakini vimelea vya Malaria vimekuwa sugu kwa dawa hiyo, kwa mujib wa Grant Dorsey, mtaalam wa magonjwa ya kuambukiza katika chuo kikuu cha Carlifornia mjini San Fransisco.

Bw. Dorsey anasema,wameacha kuitumia kama dawa, kwa zaidi ya mwongo mmoja sasa kwa sababu imekuwa sugu. Hata hivyo, bado tunaitumia kuzuia Malaria kwa wanawake wajawazito. Kwa hivyo hio ndio ilikuwa fikra zetu kutokana na utafiti, kuwa dawa hii inayopendekezwa kuzuia Malaria katika wanawake wajawazito huwenda ikawa haifanyi kazi.

Watafiti wamekuwa wakiifanyia majaribio dawa iitwayo: Dihdroartemisininpiperaquine.

Katika utafiti ulochapishwa kwenye jarida la New England Journal of Medicine, Bw. Dorsey na wenzake wanaripoti kuwa matibabu ya dawa mchanganyiko hupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya Malaria katika kundi la wanawake mia 3 nchini Uganda, ambao hamna kati yao alokuwa amewahi kuambukizwa pale utafiti huo ulipoanza.

Baadhi ya wanawake walipewa dozi 3 katika kipindi cha ujauzito wao, na wengine walipewa mara moja kwa mwezi. Kundi la tatu walipewa dawa kwa kawaida yake.

Bw Dorsey anasema, hatari ya kuambikizwa na Malaria wakati ukiwa mja mzito imepunguwa kwa asli mia 17, na kama dawa wakipewa mara moja kwa mwezi basi maambukizo yanagunguwa kwa asli mia 5.Kwa hiyo hatari ya kuwa na vimelea vya Malaria wakati mwanamke akiwa mja mzito imepungua kutoka asli mia 40 hadi asli mia 17.

Shirika la afya duniani limependekeza utafiti mkubwa zaidi kufanywa kutazama ufanisi wa dawa ya Dihydroartemisininpiperarquinine, kabla kuipendekeza katika kuzuia Malaria katika wanawake wajawazito.

XS
SM
MD
LG