Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:16

Baba Mtakatifu Francis amaliza ziara ya Marekani


Mtoto aliyebebwa kutoka kundi la watt amgusa Papa Francis mjini Philadelphia, Sept. 27, 2015.
Mtoto aliyebebwa kutoka kundi la watt amgusa Papa Francis mjini Philadelphia, Sept. 27, 2015.

Baba Mtakatifu Francis alimaliza ziara yake Marekani kwa kuendesha misa ya mchana mjini Philadelphia, akihimiza maelfu ya waliohudhuria kutunza familia zao na kuonyesha watoto wao mifano ya upendo na matunzo.

Katika siku ya sita na ya mwisho ya ziara yake ya kihistoria nchini Marekani Papa Francis alihimiza waumini waliohudhuria misa ya wazi katika uwanja wa Benjamin Franklin Parkway mjini Philadelphia kupokea changamato ya kulinda "nyumba yetu" - dunia.

Alitoa wito wa kujumuisha "familia yote ya dunia katika kupata maendeleo endelevu."

Watu wakikusanyika katika Benjamin Franklin Parkway kabla ya misa Philadelphia Jumapili, Sept. 27, 2015.
Watu wakikusanyika katika Benjamin Franklin Parkway kabla ya misa Philadelphia Jumapili, Sept. 27, 2015.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia alitoa wito kwa waumini kuondoa tofauti kati ya jamii. "Tunaomba watoto wetu watuone kama mifano ya umoja sio mgawanyiko."

Mkazo wa Papa Francis kwa watoto unafuatia azimio lake mapema asubuhi kuwa kanisa katoliki litafanya juhudi za hali ya juu kuzuia na kulipa kwa maovu waliyotendewa watoto katika kashfa ya unyanyasaji wa kingono iliyokumba kanisa hilo miaka ya nyuma.

Baada ya misa hiyo Papa Francis atakutana na Makamu Rais wa Marekani Joe Biden kabla ya kuanza safari ya kurudi nyumbani Vatican.

XS
SM
MD
LG