Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 23:39

Polisi wa DRC wapiga marufuku mikutano Kinshasa


Watu wanapita mbele ya bango kubwa linaloonesha picha ya Rais Joseph Kabila
Watu wanapita mbele ya bango kubwa linaloonesha picha ya Rais Joseph Kabila

Mikutano ya kisiasa imepigwa marufuku Kinshasa Jumamosi baada ya mtu moja kuuliwa katikia ghasia za kampeni.

Katika siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wagombania wawili wakuu wa kiti cha rais Rais Joseph Kabila na mpinzani mkuu Etienne Tshisekedi wamekua na mikutano sambamba Jumamosi mjini Kinshasa.

Na licha ya marufuku afisa wa cheo cha juu wa chama cha Tshisekedi, UDPS amesema mkutano wao utaendelea.

Mapema Jumamosi polisi walitumia nguvu kuwatawanya mamia ya waandamanaji mjini Kinshasa na vyombo vya habari vinaripoti kuuliwa kwa mtu mmoja wakati wa ghasia zilizotokea.

Siku ya Ijuma David Pottie mfuatiliaji uchaguzi kutoka taasisi ya Carter Center, anasema mikutano hiyo ya mashindano kufanyika karibu na karibu yanazusha wasi wasi ya kuzuka ghasia kati ya wafuasi wa vyama hasimu.

Kuna wagombea 10 wanaoshindana na rais Kabila wakati wa uchaguzi wa rais na bunge utakaofanyika Jumatatu, na kuna wagombea elfu 18 wanaogombania viti 500 vya bunge la taifa.

XS
SM
MD
LG