Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:14

Polisi 302 wafutwa kazi Kenya


Tume ya taifa ya Polisi nchini Kenya, imewafuta kazi maafisa 302 wa polisi kushindwa kufika katika zoezi la ukaguzi wa utendaji kazi wao.

Mwenyekiti wa tume hiyo ya polisi Johnston Kavuludi akiwa ameambatana na mkuu wa jeshi la polisi la Kenya, Joseph Boinnet, alitangaza Alhamisi kwamba vyeo vya polisi hao ni kuanzia Konstebo mpaka Mainpekta wakuu.

Kavuludi amesema maamuzi hayo yalifikiwa na tume hiyo Juni 7, na kusema tangazo hilo linawahusu wale wote waliokataa kufika wakati wa zoezi la ukaguzi, wale waliopuuzia simu mwito wa tume, na wale walioshindwa kuwasilisha nyaraka muhimu zilizo hitajika.

Zoezi hilo la ukaguzi kwa maafisa wa polisi lililenga kuleta imani ya umma kwa jeshi lenye dhamana ya kulinda wananchi pamoja na mali zao ikiwa na kuhakikisha linasimamia sheria.

Licha ya kwamba ni uamuzi mgumu, mwenyekiti huyo wa tume amesema hakukuwa na chaguo lingine zaidi ya kufuta ajira zao kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa na lazima, lakini lilipuuziwa ambapo maafisa wengine waligoma hata kuwasiliana na tume.

Zoezi hilo bado linaendelea kufanyika katika maeneo mengine ya nchi.

Unaweza kusikiliza ripoti ya mwandishi wetu Josephat Kioko, kutoka Kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG