Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:57

AU yawaalika Gbagbo na Ouattara kwenda Ethiopia


Laurent Gbagbo, Rais wa Ivory Coast anayeng'ang'ania madaraka.
Laurent Gbagbo, Rais wa Ivory Coast anayeng'ang'ania madaraka.

Mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika amehitimisha mazungumzo yake huko Ivory Coast kwa kuwaalika marais waliohasimiana nchini humo katika mkutano huko Ethiopia ili kusulihisha mgogoro wao wa kisiasa.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Jean Ping aliondoka mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan, baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwa nyakati tofauti na Rais anayeng’ang’ania madaraka Laurent Gbagbo na mshindi anayetambuliwa na Umoja wa Mataifa katika uchaguzi wa Novemba, waziri mkuu wa zamani Allassane Ouattara.

Ping alikwenda Abidjan akiwa na ujumbe toka kwa marais wa Burkina Faso, Chad, Mauritania, Afrika Kusini na Tanzania. Viongozi hao watano wanaunda jopo la Umoja wa Afrika lililopewa jukumu la kutatua mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast ifikapo mwisho wa mwezi Machi.

Katika ziara yake huko Abidjan, Ping hakueleza bayana ujumbe huo, lakini aliwaalika Bw. Gbagbo na Bw. Ouattara katika mazungumzo yanayodhaminiwa na Umoja wa Afrika huko Addis Ababa, Alhamis ya wiki hii.

Bw. Ouattara amesema anapanga kuhudhuria tukio hilo. Ikiwa atafanya hivyo, hii itakuwa ni mara ya kwanza kuondoka katika hoteli yake iliyozingirwa huko Abidjan ambako amekuwa akiishi tangu matokeo ya uchaguzi yatangazwe mwanzoni mwa mwezi Disemba.

Mpaka sasa hakuna majibu yeyote toka kwa Bw Gbagbo ama kutoka kwa mkuu wa baraza la katiba la Ivory Coast, Paul Yao N’Dre, ambaye pia amealikwa.

XS
SM
MD
LG