Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:56

Pence: 'Ahadi ya Marekani Kwa NATO ni Yakudumu'


Makamu wa Rais Mike Pence akizungumza kwenye mkutano wa usalama Munich, Ujerumani, Feb. 18, 2017.
Makamu wa Rais Mike Pence akizungumza kwenye mkutano wa usalama Munich, Ujerumani, Feb. 18, 2017.

Makamu wa Rais amesema katika Mkutano wa Usalama wa Munich “Historia itashuhudia kwamba Marekani na Ulaya zimekuwa na amani na mafanikio, na sisi ndio tunasaidia kupeleka mbele amani na mafanikio hayo ulimwenguni.”

Mike Pence amesema Jumamosi, “Hivi leo, kwa niaba ya Rais Trump, ninawahakikishia nia yetu ya kuendeleza hili. Marekani itaendelea kuisaidia NATO kwa nguvu zote na hatutarudi nyuma katika dhamira yetu kwenye ushirikiano huu kati ya nchi zilizo pande mbili za bahari ya Pacific.

“Hatma ya Marekani na Ulaya imefungamana,” makamu wa rais amesema. “Mshikamano wetu ni wenye nguvu kwa zaidi ya karne moja, na Wamarekani wamekuwa mbele kutoka katika nchi yao kuja kuwasaidia katika ulinzi wenu.”

Pence amesema NATO “Lazima tuwe mstari wa mbele katika ulimwengu wa mawasiliano ya mtandao wa kisasa kama vile tulivyo katika ulimwengu wa maisha yetu ya kawaida” katika kupambana na makundi ya Islamic State, ambayo amesema “pengine ndio uovu mkubwa kuliko yote” na imeonyesha ukatili ambao haujawahi kuonekana tangia zama hizo ambako hakukuwa na ustaarabu.

“Na kuhusu Ukraine,” makamu wa rais amesema, “ni lazima tuiwajibishe Russia na kuwataka waheshimu mkataba wa Minsk, wakianza na kuzuia vitendo vya kuvunja amani vinavyoendelea upande wa mashariki ya Ukraine."

Amesema Marekani “itaendelea kuiwajibisha Russia, pamoja na kuwa tunatafuta maeneo mapya ya ushirikiano nao, ambao nyote mnatambua kwamba Rais Trump anaamini unaweza kupatikana."

XS
SM
MD
LG