Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:44

Marais wa Marekani hutoa hotuba kutokea Oval kwa Matukio Muhimu


Picha hii iliyotolewa na Ikulu ya Marekani inamuonyesha, Rais Barack Obama akiipitia hotuba yake kwenye Oval Office kabla ya kuitoa kupitia televisheni, Mei 1, 2011.
Picha hii iliyotolewa na Ikulu ya Marekani inamuonyesha, Rais Barack Obama akiipitia hotuba yake kwenye Oval Office kabla ya kuitoa kupitia televisheni, Mei 1, 2011.

Rais wa Marekani, Barack Obama Jumapili usiku amezungumza na wamarekani kuelezea mapambano ya utawala wake dhidi ya magaidi ikiwa ni pamoja na kundi la wanamgambo wa kiislamu la Islamic State. Amezungumza kutokea kwenye ofisi yake ya katika Ikulu ya Marekani.

Kwa kawaida hotuba inayoonyeshwa kitaifa ambayo hutolewa kutoka kwenye ofisi ya Rais wa Marekani maarufu kama Oval Office kutoka Ikulu ya White House, inaelezewa ni hotuba ambayo inakuwa ni moja ya matukio makuu kwa umuhimu wa kitaifa na kimataifa.

Baadhi ya matukio muhimu ambayo marais wa Marekani waliitumia Oval Office kuzungumza na watu wa Marekani na jumuiya ya kimataifa ni yafuatayo.

1947 – Rais Harry S. Truman alitoa hotuba kuwasihi wamarekani kuhifadhi chakula ili kuisaidia Ulaya iliyokuwa inatoka vitani.

1957 – Rais Dwight D. Eisenhower alitoa hotuba kuwajulisha wamarekani kuhusu uamuzi wake wa kupeleka majeshi huko Little Rock, Arkansas kuimarisha dhidi ya ubaguzi katika shule.

1962 – Rais John F. Kennedy alitoa hotuba kuhusu mzozo wa kombora la Cuba.

1986 – Rais Ronald Reagan alitoa hotuba kufuatia maafa kwenye chombo cha anga ya juu – Space Shuttle Challenger.

2001 – Rais George W. Bush jioni ya siku ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 aliwahutubia wamarekani.

2010 – Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza alilihutubia taifa kuhusu umwagikaji mkubwa wa mafuta kwenye Ghuba ya Mexico. Hotuba hii aliitoa Juni 15.

2010 – Agosti 31 Rais Obama alizungumza tena kutokea Oval Office akizungumzia kuhusu kumaliza operesheni za jeshi la Marekani nchini Iraq na kuwakumbusha watu wa Marekani kuhusu ahadi yake ya kumaliza vita.

Hotuba ya Desemba 6, 2015 ilikuwa ni ya tatu ya Rais Obama kuzungumza na taifa kutokea Oval Office.

Rais Bill Clinton alitoa hotuba kutoka Oval Office mara 13, Rais George H. W. Bush alitoa hotuba mara 11 kutokea ofisi hiyo na Rais Ronald Reagan yuko juu kwenye orodha ya marais wa Marekani waliotoa hotuba kutokea Oval Office. Yeye alilihutubia taifa mara 16 kutoka kwenye ofisi hiyo.

XS
SM
MD
LG