Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 03:42

Serikali ya Ouattara yaunda jeshi jipya Ivory Coast


Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara(R) akipeana mkono na Jenerali Philippe Mangou, kwenye hoteli ya Golf mjini Abidjan.
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara(R) akipeana mkono na Jenerali Philippe Mangou, kwenye hoteli ya Golf mjini Abidjan.

Serikali mpya ya Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara inaandikisha wanajeshi wapya kuboresha hali katika mji mkuu wa kibiashara Abidjan baada ya miezi minne ya ghasia za kisiasa. Habari zaidi zinasema maisha yameanza kurudi katika hali ya kawaida ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kukamatwa kwa rais wa zamani nchini humo, Laurent Gbagbo.

Katika mapigano ya kumuweka madarakani Ouattara baada ya kushinda uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba mwaka jana, makundi ya vijana yanayomuunga mkono Ouattara yalizidi katika maeneo ya Abidjan kukabiliana na jeshi la rais wa zamani, Gbagbo.

Hivi sasa baadhi ya wanamgambo wa Ouattara wanayo nafasi ya kujiunga na serikali mpya ya Ouattara kama wanajeshi na polisi.

Mwalimu wa mafunzo katika kundi jipya la Repuplican Forces nchini Ivory Coast, Yaya Cisse, anasema hawa ni raia ambao watapatiwa mafunzo kuwa wanajeshi kamili. Wale ambao wanataka kuwa polisi wataendelea. Wale ambao wanataka kuacha, anasema tutawaruhusu kufanya hivyo.

Kuweka sawa huduma za usalama nchini Ivory Coast ni sehemu kubwa ya kurudisha tena ushwari katika mji mkuu wa kibiashara ambapo Rais Ouattara anataka kuanza haraka uuzaji wa kakao nje ya nchi, kufungua tena mabenki na kukufua tena viwanda ili uchumi wa nchi usonge tena mbele.

XS
SM
MD
LG