Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:58

Operesheni za kivita za Marekani zaisha Iraq


Rais Obama anasema jukumu jipya la Marekani nchini Iraq ni kutoa ushauri na msaada kwa vikosi vya usalama vya Iraq.

Marekani imetangaza kumalizika rasmi kwa operesheni za mapambano nchini Iraq miaka 7 na nusu tangu majeshi ya Marekani kuivamia Iraq. Akihutubia taifa Jumanne kutoka White House mjini Washington Rais Obama alitoa shukurani kwa majeshi kutokana na huduma zao na kutangaza kwamba jukumu lao la mapambano limekamilika.

"Operesheni Freedom imekamilika na wananchi wa Iraq hivi sasa wana wajibika kuongoza jukumu la usalama wa nchi yao," alisema rais Obama.

Ikiwa ni mara ya pili kwa rais kutumia afisi yake kulihutubia taifa tangu kuchukua madaraka, Bw. Obama hakutangaza ushindi, lakini alisema hatua ya kuelekea majukumu mapya inachukuliwa hivi sasa.

"Kupitia ukurasa huu muhimu katika historia ya Marekani na Iraq, tumetekeleza wajibu wetu na wakati umefika kugeuza ukurasa," alisema rais Obama.

Kiasi ya wanajeshi elfu 50 wa Marekani watabaki Iraq ambapo wanatarajiwa kuondoka mwishoni mwa mwaka ujao.

Rais alisema jukumu jipya la Marekani litakua ni kutoa ushauri na kuvisaidia vikosi vya usalama vya Iraq kushirikiana na vikosi vinavyopambana na ugaidi na kulinda raia.

Wanajeshi wa kiiraq.
Wanajeshi wa kiiraq.

Bw. Obama alisema raia wengi zaidi wa Marekani wataunga mkono juhudi za Iraq kuunda serikali na kurudi katika hali ya kawaida baada ya miaka ya vita.

" WaIraq pekee ndio wanaweza kubuni mfumo wao wa kidemokrasia ndani ya mipaka yao. Kile Marekani inachoweza kufanya na itafanya, ni kuwapatia msaada wananchi wa Iraq kama rafiki na mshirika," rais Obama alisema.

Ikiwa ni karibu miezi sita baada ya uchaguzi wa Iraq, rais obama aliwahimiza viongozi wa nchi hiyo kufanya kwa nia ya dhati na kwa dharura kuunda serikali mpya.

Rais Obama aliahidi msaada kwa Iraq, na kusema kuwa baadhi ya majeshi ya Marekani yana hamishwa kutoka Iraq hadi Afghanistan, ambako wanapambana na Taliban na Al Qaida kwa karibu miaka kumi. Rais alisema Marekani itawashinda Al Qaida na kuzuia Afghanistan kutumbukia tena na kuwa kituo cha ugaidi.

XS
SM
MD
LG