Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:18

Ocampo aomba msaada wa Umoja wa mataifa kumkamata Bashir .


Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo akipiga picha baada ya mahojiano na waandishi.
Mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo akipiga picha baada ya mahojiano na waandishi.

Ocampo alitaka Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhimiza nchi kukamata viongozi wa Sudan walioshitakiwa.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, imewashitaki maafisa wanne wa Sudan kwa uhalifu wa kivita huko Darfur. Watu hao ni pamoja na rais wa Sudan Omar al Bashir, na waziri wa ulinzi Abdul Rahim Hussein. Lakini hakuna mtu aliokamatwa hadi sasa.

Mwendesha mashtaka mkuu aliliambia baraza la usalama kuwa kwa kutekeleza hati za kukamatwa kutaleta mabadiliko makubwa kwa Darfur, na kukosa kwa kukamatwa kwa watu hao wanne, ni changamoto ya moja kwa moja kwa mamlaka ya baraza hilo.

Alisema sio jukumu la vikosi vya kuweka amani wa umoja mataifa huko Sudan wajulikanao pia kama UNAMID, kuwakamata watu hao.

Balozi wa Sudan , Daffa Alla Elhag Ali Osman, akizungumza kupitia mkalimani, alipinga wazo la mwendesha mashtaka Ocampo, na kumshutumu kwa kudharau mkataba wa umoja mataifa.

Mwakilishi wa Marekani Jeffrey De Laurentis, alisema taifa lake lina wasiwasi mkubwa juu ya hali huko Sudan, na jukumu ambalo kuendelea kwa kutoshtakiwa kwa uhalifu uliofanyika huko Darfur limeendelea kuchelewesha kuwepo kwa amani ya kudumu.

Mwishoni mwa mkutano wa baraza la usalama, mwendesha mashtaka Ocampo aliliambia baraza hilo kuwa anamtahadharisha balozi wa sudan, kwamba kwa kukana mashtaka dhidi ya maafisa wa Sudan, anaweza pia kuwa anahusika katika uhalifu huo. Naye Bw. Osman alijibu matamshi ya Ocampo kwa kusema kuwa ni ukikaji wa sheria za kidiplomasia na kisiasa, na ni matamshi ya gaidi.

Mahakama ya ICC ilimshtaki rais wa Sudan kwa uhalifu wa kivita, na uhalifu dhidi ya binadam hapo mwaka 2009, ikisema alipanga kampeni ya mauaji, ubakaji na uhalifu mwingine dhidi ya binadam huko Darfur.

XS
SM
MD
LG