Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:18

Rais Obama aomba kura za vijana

Rais Obama katika harakati za kampeni za uchaguzi ujao, wa Novemba 2.
Rais Obama katika harakati za kampeni za uchaguzi ujao, wa Novemba 2.

Rais wa Marekani Barack Obama yupo katika harakati za kampeni kwa siku mbili kuwarai wapiga kura vijana kuunga mkono chama cha Democrat, kinachohitaji kulinda wingi wa wawakilishi wake bungeni.

Rais wa Marekani Barack Obama yupo katika harakati za kampeni kwa siku mbili kuwarai wapiga kura vijana kuunga mkono chama cha Democrat, kinachohitaji kulinda wingi wa wawakilishi wake bungeni.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika chuo kikuu cha Wisconsin Jumanne, Rais aliwataka wapiga kura vijana waliopo vyuoni kusaidia kuokoa chama cha Democrat, kisianguke katika uchaguzi ujao wa Novemba 2.

Miaka miwili iliyopita, bwana Obama alisema wapiga kura vijana wanatoa changamoto ya pamoja hapa Washington, kwa kusaidia kumchagua yeye kuwa rais. Alisema kama kila mmoja ambaye alipigania mabadiliko mwaka 2008, atajitokeze kupiga kura mwezi Novemba, chama cha Democrat kitashinda.

Viongozi wa chama cha Republican wana shauku kuhusu mtazamo wao katika kile walichokiita uchaguzi mdogo ambao unaangukia kati kati ya kinyang’anyiro cha rais cha mwaka 2008 na 2012.

Chama cha upinzani kina wawakilishi wengi kote katika bunge, lakini wachambuzi wengi wa masuala ya siasa wanasema wanaweza kubadilika mwaka huu katika kudhibiti baraza moja au mabaraza yote mawili ya bunge.

XS
SM
MD
LG