Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:51

Obama atembelea msikiti kwa mara ya kwanza Marekani


U.S. President Barack Obama greets students after his remarks at the Islamic Society of Baltimore mosque in Catonsville, Maryland, Feb. 3, 2016.
U.S. President Barack Obama greets students after his remarks at the Islamic Society of Baltimore mosque in Catonsville, Maryland, Feb. 3, 2016.

Rais Barack Obama wa Marekani Jumatano alifanya ziara yake ya kwanza katika msikiti nchini Marekani tangu aingie madarakani na kutumia ziara hiyo kupinga kauli zinazotolewa hasa wakati huu wa uchaguzi dhidi ya waislamu.

Ziara hiyo katika msikiti mmoja wa mjini Baltimore katika jimbo la Maryland Obama alisema "Wamarekani waislamu wanatuweka salama," akitoa sifa kwa michango wa waislamu katika jamii zao. "Ni polisi wetu, zima moto wetu. Wako katika wizara ya ulinzi na usalama," alisema.

Msikiti huo wa Islamic Society of Baltimore umekuwepo kwa miaka 47 na una maelfu ya waumini. Obama alisema michango kadha inayofanywa na waislamu huku akipinga vikali lugha inayotumiwa na wagombea urais warepublican kama Donald Trump.

Obama ametembelea misikiti katika siku za nyuma lakini sio ndani ya Marekani ambako kuna waislamu karibu millioni tatu, kulingana na kituo cha utafiti cha Pew. Makundi mengi ya kiisalmu yamekuwa yakimwomba atembelee msikiti ndani ya Marekani ili kuonyesha upinzani dhidi ya hisia zinazopinga uislamu, kama vile Rais George Bush alivyofanya siku chache baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001.

XS
SM
MD
LG