Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:43

Obama kukutana na viongozi wa Congress


Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama
Rais Barack Obama wa Marekani amewaita viongozi wa bunge kwa mazungumzo huko White House wiki ijayo juu ya namna ya kuweza kukata matumizi ya serikali na ongezeko la kodi mwezi Januari.

Bwana Obama ambaye alichaguliwa tena kuongoza muhula wa pili wa miaka minne aliuambia mkusanyiko huko White House kwamba nchi inahitaji haraka kujenga umoja ili kutatua matatizo yake ya kifedha, na kipaumbele cha kuhamasisha ajira na ukuaji wa uchumi.

Bwana Obama alisema inahitajika kudhibiti matumizi ya serikali. Lakini aliongeza kuwa hatuwezi kupata mafanikio kwa kupunguza tu matumizi katika mipango ya serikali.

Alisema uchaguzi ulionyesha kwamba wamarekani wengi wanaidhinisha mpango wake wa kuongeza kodi kwa matajiri, familia kama zile zinazotengeneza zaidi ya dola 250,000 kwa mwaka. Wapinzani wake wa chama cha Republican bungeni wanapinga mpango wowote wa kuongeza kodi unaotakiwa kuanza mwaka mpya.

Marekani inakabiliwa na kile Washington inachokiita “fiscal cliff” ukataji matumizi wa lazima wa dola bilioni 600 ili kuokoa program za taifa na ongezeko la kodi ambalo litawa-athiri wafanyakazi wote wa Marekani ifikapo Januari mosi.

Wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi wana wasi wasi wa ukataji na ongezeko la kodi, kama jambo hilo likitokea, linaweza kurudisha hali ya uchumi kuwa mbaya.

Awali spika wa bunge, m-Republican John Boehner aliwaambia waandishi wa habari kwamba kuongeza kiwango cha kodi kutazorotesha uwezo wa kubuni ajira ambazo kila mmoja anazitaka. Alisema suala la uchumi lilikuwa kipaumbele kwa wapiga kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika wiki hii.

Boehner alisema mwaka 2013 unatakiwa kuwa mwaka wa serikali kuanza kutatua matatizo yake ya kifedha hasa masuala ya madeni, kodi na matumizi kwa pensheni ya serikali na huduma ya afya kwa wazee.

Boehner anasema yupo wazi kwa baadhi ya mabadiliko ya kuongeza mapato mapya ya serikali, iwapo yanajumuisha mabadiliko kwa pensheni na program za huduma ya afya.
XS
SM
MD
LG