Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:43

Obama awasihi wamarekani kupima HIV


Baadhi ya vidonge vinavyopunguza makali ya maambukizo ya HIV vinavyotumiwa na waathirika wanaoishi na virusi vya HIV duniani
Baadhi ya vidonge vinavyopunguza makali ya maambukizo ya HIV vinavyotumiwa na waathirika wanaoishi na virusi vya HIV duniani

Rais Barack Obama amewasihi wamarekani kwenda kupima HIV. Katika taarifa ya Jumatatu juu ya siku ya kitaifa ya HIV, Rais amesema mtu mmoja kati ya wamarekani watano anaishi na HIV na hajui kama ameambukizwa. Ameelezea umuhimu wa kuhakikisha watu wanafahamu hali zao za afya, pamoja na kupata matibabu kwa wale ambao wana virusi ili kulinda afya zao na kuzuia maambukizo zaidi.

Rais alisema ni miongo mitatu sasa tangu kesi ya kwanza ya HIV na ukimwi ilipogundulika na kwamba katika kipindi hicho wamarekani 600,000 wamefariki kutokana na tatizo hilo, huku zaidi ya wamarekani milioni moja wanaishi na virusi vya ugonjwa huo.

HIV ni virusi ambavyo vinasababisha ugonjwa wa ukimwi. Umoja wa Mataifa unasema unakadiria watu milioni 34 duniani wanaishi na HIV na watu wapatao milioni 30 ulimwenguni kote wamekufa na magonjwa yanayohusiana na ukimwi katika kipindi cha miaka 30 tangu kesi ya kwanza ya ugonjwa huu iliporipotiwa.

XS
SM
MD
LG