Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 23:07

Obama akutana na viongozi wa Afrika


Rais wa Marekani Barack Obama akizungumzia masuala ya biashara kati ya Marekani na Afrika, Washington, August 5, 2014.
Rais wa Marekani Barack Obama akizungumzia masuala ya biashara kati ya Marekani na Afrika, Washington, August 5, 2014.

Rais wa Marekani Barack Obama na viongozi wa Afrika wameanza mazungumzo mjini Washington jumatano kuhusu kupanua biashara, kuimarisha usalama na kuboresha uwajibikaji wa serikali kote barani Afrika.

Mazungumzo hayo ni katika mifululizo ya mikutano iliyofanyika jumatano ikiwa ni kilele cha mkutano mkubwa wa siku tatu unaowashirikisha wakuu wa mataifa 50 kutoka barani Afrika. Katika matamshi yake ya ufunguzi hapo jumatano, bwana Obama alisema Afrika mpya inajitokeza. “Huku baadhi ya chumi zikikua haraka sana duniani, ukuaji wa daraja la kati na vijana na ukuaji wa haraka sana wa idadi ya watu duniani, Afrika itasaidia kujenga muundo wa dunia ambao haujawahi kuwepo awali”.

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

​Rais alisema kuongezeka fursa za biashara barani Afrika kutasaidia kuandaa uhusiano kati ya Marekani na bara la Afrika. “Wakati umefika kuwa na mtazamo mpya wa urafiki kati ya Amerika na Afrika, urafiki wa usawa ambao unalenga uwezo wa Afrika wa kutatua matatizo na uwezo wa Afrika wa kukua na ndio sababu tupo hapa”.

Jumanne jioni White House iliwaalika wageni chakula cha jioni ambapo Rais alieleza asili yake ya kiafrika na alisema kwamba kwa familia yake uhusiano kati ya Marekani na Afrika ni wa kibinafsi sana.

Awali bwana Obama alitangaza dola bilioni 33 katika uwekezaji binafsi na wa umma nchini Marekani kwa mataifa mbali mbali barani Afrika.

XS
SM
MD
LG