Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:16

Obama Akutana na Maafisa wa BP


Rais Obama akutana na maafisa wa BP leo White House kudai walipie gharama za uharibifu wa uvujaji mafuta Ghuba ya Mexico.

Rais Barack Obama wa Marekani anakutana na maafisa watendaji wa shirika la mafuta la BP leo katika White House mjini Washington ambapo anatazamiwa kudai kampuni hiyo ilipie gharama za uharibifu wa mazingira uliosababishwa na uvujaji mafuta katika Ghuba ya Mexico nchini Marekani.

Katika hotuba yake kwa taifa Jumanne usiku Rais Obama alisema atadai kampuni ya BP itenge kiwango kikubwa kwa ajili ya fidia kwa wale walioathirika kwa kile alichoita "uzembe" wa kampuni hiyo.

Uvujaji wa mafuta ulianza Aprili 20 ulipotokea mlipuko katika mtambo wa kuchimbia mafuta baharini katika mwambao wa jimbo la Louisiana. Obama alielezea uvujaji huo kuwa mkasa mkubwa wa kimazingira kuliko yote ambayo imewahi kuipata Marekani.

Baada ya hotuba ya Obama Jumanne usiku BP ilitoa taarifa ikisema inakubaliana na lengo la Rais kusafisha eneo hilo na kusaidia wale walioathirika. Baadhi ya wabunge wa Marekani wanataka BP itenge karibu dolla billioni 20 kwa ajili ya mfuko maalum wa fidia.

XS
SM
MD
LG