Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:13

Obama ahutubia maelfu Washington


Rais Barack Obama, Mkewe Michelle Obama, marais wa zamani Jimmy Carter na Bill Clinton
Agosti 28, 2013
Rais Barack Obama, Mkewe Michelle Obama, marais wa zamani Jimmy Carter na Bill Clinton Agosti 28, 2013
Akizungumza na maelfu ya watu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 tangu maandamano ya kutetea haki za kiraia kufanyika jijini Washington, rais Barack Obama jana Jumatano alisema ‘kazi haijamalizika’ ya kutetea haki na usawa kwa wamarekani wote.

Miaka 50 baada ya Mchungaji Martin Luther king Jr. kutoa hotuba ya kihistoria na ya kusisimua akisema; “I have a dream” wakati wa ubaguzi mkubwa wa rangi Marekani, rais wa kwanza mweusi Marekani alisimama katika ngazi zile, zile alizosimama kwenye mnara wa kumbukumbuku wa Lincoln Memorial.

Bw. Obama alielezea wasifu wa Dr.King pamoja na kujitolea kafara kwa walioshiriki maandamano makubwa ya Washington miaka 50 iliyopita. Alisema kutokana na maandamano yao, sheria ya haki za kiraia ilipita. Na kwa sababu waliandamana sheria ya haki za kupiga kura ilitiwa saini na kwa sababu hiyo hiyo wasichana na wavulana weusi wanaweza kuishi maisha yao kikamilifu bila kuwa watumwa wa mtu mwingine.

Rais Obama aliendelea kusema na kwa sababu waliandamana, hata White House imebadilika huku maelfu ya watu wakimshangilia. Bw. Obama alisema maandamano hayo yalileta haki sio tu kwa wamarekani weusi lakini kwa watu wa rangi nyingine Marekani na duniani waliokuwa na kiu cha kuwa huru.

Alisema mengi yamebadilika tangu maandamano hayo ya mwaka wa 1963 lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanywa. Alisema kuna mwanya mkubwa kati ya matajiri na maskini miongoni mwa watu wa rangi mbalimbali Marekani na migawanyiko mikubwa ya kisiasa hapa Washington inayofanya ndoto ya Martin Luther King Jr. kuonekana kuwa mbali sana kutimia.

Rais Obama alisema Marekani ina chaguo, ama kuendelea na msukumo huu mkubwa wa kidemokrasia, au kuzembea na kukifanya kizazi kijacho kuishi bila matumaini au kujikakamua na kufanya mabadiliko ya kuleta usawa na haki kwa wote.

Orodha ya waliotoa hotuba katika maadhimisho hayo ilikuwa ndefu, na ilijumwisha mwana wa kike wa Dr. King, mchungaji Bernice King, marais wa zamani Bill Clinton, Jimmy Carter, wacheza sinema maarufu na hata watangazaji mashuhuri wa televisheni. Mbunge John Lewis mmoja wa viongozi wa maandamano ya kutetea haki za kiraia mwaka wa 1963 alisema ingawa kuna maendeleo, ubaguzi wa rangi ungali umejikita katika jamii ya wamarekani.
XS
SM
MD
LG