Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:52

Obama aelekea ulaya kushauriana na washirika wa NATO


Rais Obama akipunga mkono tayari kuelekea safari yake ya ulaya kukutana na washirika wa NATO
Rais Obama akipunga mkono tayari kuelekea safari yake ya ulaya kukutana na washirika wa NATO

Rais wa Marekani Barack Obama ameondoka Washington kwa ziara ya ziku nne huko ulaya iliyolenga kuwahakikishia washirika wa NATO uungaji mkono wa Marekani, huku mivutano ya kieneo juu ya jukumu la Russia huko Ukraine ikiendelea kuongezeka.

Bwana Obama atafanya mazungumzo ya siku nzima hapo jumatano katika mji mkuu wa Estonia na marais wa Estonia, Latvia na Lithuania.

Mikutano huko Tallinn, kilomita 200 kutoka mpaka wa Russia inafanyika ikiwa ni majibu kwa ongezeko la wasiwasi kuhusu kuhusika kwa jeshi la Russia huko Ukraine na uwezekano wa vitisho vya Russia kwa mataifa ya Baltic. Rais ameelezea mazungumzo ya Baltic yanamaanisha kuonesha mataifa hayo Jamhuri tatu za zamani za Kisovieti kwamba tunamaanisha kile tunachosema kwa kuheshimu majukumu yetu katika mkataba.

XS
SM
MD
LG