Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:37

Nunes akataa kujitoa katika uchunguzi wa Russia


Devin Nunes
Devin Nunes

Kamati ya Usalama ya Bunge la Marekani imesitisha mikutano yote wiki hii kutokana na mwenyekiti wake Devin Nunes kukataa kujiondoa katika uchunguzi wa Russia.

Mwenyekiti huyo amekataa shinikizo la Wademokrat kumtaka ajitoe kutoka katika kamati hiyo inayo ichunguza Russia juu ya kuvuruga uchaguzi wa urais Marekani mwaka 2016.

“Kwa nini nifanye hivyo? Nunes aliwaambia waandishi Jumanne, siku moja baada ya mwenzie, kiongozi wa juu wa Kidemokrat, katika kamati hiyo, Adam Schiff kumtaka Nunes ajiuzulu.

“Hili sio pendekezo ambalo ni jepesi, kama Mwenyekiti na mimi tumefanya kazi pamoja kwa miaka kadhaa,” Schiff aliandika Jumatatu.

Aliongeza kuwa itakuwa vigumu kwa umma kuendelea kuwa na imani katika uchunguzi huu kama hautakuwa ni wenye kutopendelea pande yoyote au mwenyekiti kuupeleka vile anavyotaka.”

Nunes alikutana na chanzo cha habari katika viwanja vya Ikulu ya White House kabla ya kutoa habari wiki iliyopita kuwa Rais Trump alihusishwa na mazungumzo ya kigeni yaliyokuwa yamenaswa na vyombo vya usalama, kwa mujibu wa msemaji wake Jack Langer. Langer amesema Jumatatu kwamba Nunes alitaka “ kusogea sehemu iliyokuwa salama ili kuweza kuiangalia taarifa aliyokuwa anapewa na mtu huyo.

Kabla ya hapo, Nunes alikuwa hataki kusema mahali alipokutana na chanzo hicho, na mpaka sasa hajamtambulisha mtu huyo.

Nunes alizungumza na waandishi na rais kuhusu nyaraka hizo nyeti wiki iliyopita bila ya kuwaarifu wanakamati wenzie wa Kamati ya Usalama ya Bunge, akiwakasirisha Wademokrat katika kamati hiyo ambao walikuwa na wasiwasi na ukweli wake. Nunes baadae aliomba radhi kwa kamati kwa kutowapa taarifa hizo za Trump mwanzoni.

“Tunajaribu kupata nyaraka hizo mapema iwezekanavyo,” Nunes aliiambia VOA Jumanne katika juhudi za kuwapa muhtasari huo wanakamati wengine.

XS
SM
MD
LG