Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 21:17

UM: Hali ya Njaa inaendelea kuwa mbaya Somalia


Mtoto aliyeathiriwa sana na baaa la njaa kutoka Somalia kusini
Mtoto aliyeathiriwa sana na baaa la njaa kutoka Somalia kusini

Wasomalia waendelea kukabiliwa na njaa licha ya misaada

Umoja wa Mataifa unasema chakula cha msaada kimegawiwa zaidi ya nusu ya Wasomali walioathiriwa na njaa, lakini hali ingali tete kuweza kukidhi mahitaji ya chakula kwa raia hao ifikapo mwaka ujao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu shughuli za kibinadamu, inasema zaidi ya wasomali milioni 2.2 wamepokea chakula cha msaada, haswa katika maeneo ya kusini mwa nchi yaliyoathiriwa zaidi na njaa.

Hata hivyo, ofisi hiyo inasema Wasomali wengine takriban milioni mbili bado wanahitaji msaada wa dharura wa chakula. Ofisi hiyo imeongeza kuwa ingawa mvua zinatarajiwa, mzozo wa chakula utaendelea hadi hapo mwakani.

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yanaendelea kuongeza juhudi zao kuwalisha raia wengi wa Somalia katika maeneo hayo ya kusini mwa Somalia lakini wanakabiliawa na vitisho vya kundi la wanamgambo wa Al-shabab.

Mashirika mengi ya kigeni yanayotoa misaada yamepigwa marufuku kuingia katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo la Al-Shabab.

XS
SM
MD
LG