Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:40

Nigeria yakanusha maafisa wa jeshi wameshtakiwa


Maafisa wa Nigeria wanakanusha ripoti kwamba maafisa wa jeshi 15 wakiwemo majenerali 10 wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi kwa kushirikiana na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.

Gazeti moja nchini humo la The Leadership liliripoti kuwa maafisa hao walikutwa na hatia ya kutoa taarifa na silaha kwa kundi la wanamgambo wenye msimamo mkali ambalo linadaiwa kusababisha maelfu ya vifo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Jumatano, maafisa wawili, msemaji wa jeshi, Meja Jenerali Chris Olukolade na ofisa mawasiliano wa serikali Mike Olmeri wote waliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba taarifa hiyo sio ya kweli.

Serikali ya Nigeria inapambana kuweza kulidhibiti kundi la Boko Haram licha ya amri ya dharura iliyotangazwa huko kaskazini-mashariki na kupelekwa kwa maelfu ya wanajeshi katika eneo. Kundi la Boko Haram limeshambulia mashule, masoko, nyumba za ibada na vituo vya jeshi.

Mashahidi wanasema wanamgambo wakati mwingine wanavalia sare za kijeshi na mara kwa mara wana nguvu zaidi kulioko wanajeshi. Kundi la Boko Haram bado linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 waliowateka kutoka shule moja katika jimbo la Borno, tukio lililotokea kati kati ya mwezi April.
XS
SM
MD
LG