Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 08:11

Vikosi vya usalama vyafanya doria Jos

Waathirika wakiwa hospitali kufuatia mlipuko wa mabomu uliotokea huko Jos, Nigeria kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismas
Waathirika wakiwa hospitali kufuatia mlipuko wa mabomu uliotokea huko Jos, Nigeria kwenye mkesha wa sikukuu ya Krismas

Mji wa Jos katikati ya Nigeria unaripotiwa kuwa tulivu huku vikosi vya usalama vikifanya doria kwenye mitaa kufuatia mabomu ya Ijumaa ambayo yaliuwa watu 32 na kujeruhi wengine 74.

Mji wa Jos katikati ya Nigeria unaripotiwa kuwa tulivu huku vikosi vya usalama vikifanya doria kwenye mitaa kufuatia mabomu ya Ijumaa ambayo yaliuwa watu 32 na kujeruhi wengine 74.

Wengi wa waathirika walikuwa wakinunua bidhaa dakika za mwisho kabla ya sikukuu ya Krismas. Mabomu yaliyotokea mkesha wa sikukuu ya Krismas yalichochea mapigano kati ya makundi yenye silaha ya wakristo na waislam siku ya Jumapili, na kupelekea baadhi ya majengo mjini humo kuchomwa. Habari zilizoripotiwa zinasema mtu mmoja aliuwawa katika mapigano hayo.

Naibu mpelelezi wa jeshi la polisi nchini Nigeria, Abubukar Audu alisema Jumatatu kwamba vituo vidogo vinne vya polisi vimewekwa kutoka eneo hilo kuzunguka miji na alisema alisema hali huko Jos hivi sasa imeimarika.

Kamishna wa habari wa jimbo la Plateau, Gregory Yenlong, anasema hali katika mji bado ina mvutano na gavana wa jimbo Jonah David Jang anaiomba serikali kuu kuimarisha ulinzi.

Maafisa wa Nigeria wanasema mapigano yalikuwa ya kisiasa, yaliyolenga kuongeza mivutano kati ya waislam na wakristo katika harakati za uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwezi April nchini humo. Mapigano yaliyozuka awali yalihusisha makundi ya kidini na kikabila huko Jos na vijiji vinavyozunguka, ambapo yameuwa mamia ya watu.

XS
SM
MD
LG